loader
Picha

WHO yatahadharisha kasi kusambaa Corona

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitahadharisha dunia, kuwa inapaswa kujipanga kukabiliana na janga la virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa taarifa ya WHO ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo, kuwa janga lakini mataifa yote yanapaswa kujiandaa na uwezekano mkubwa wa kushambuliwa na virusi hivyo hatari kwa sasa duniani.

Tishio kubwa limezidi kutokana maambukizi kuanza kusambaa kwenye maeneo mengi nje ya China.

Wagonjwa zaidi wamezidi kuripotiwa kutoka mataifa mengine ikiwemo Korea Kusini, Italia, Iran na hadi sasa watu kwenye nchi 29 nje ya China wamethibitika kuwa na virusi hivyo.

Hadi sasa watu 2069 wameambukizwa virusi hivyo nje ya China 23 kati ya hao wamepoteza maisha.

 Asili ya ugonjwa huo ni China ambako hadi sasa watu 77, 262 wamethibitika kuambukizwa, na kati ya hao 2595 wamepoteza maisha.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba idadi ya maambukizi ya COVID-19 katika mataifa ya Iran, Italia na Korea Kusini inatia wasiwasi.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi