loader
Picha

Mwongozo wa Uwekezaji kutangaza fursa Mara

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angella Kairuki amesema kukamilika kwa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mara utasaidia kuibua na kuzitangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo na hatimaye kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje.

Akizungumza katika mkutano wa majadiliano kati ya sekta ya umma, wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa Mara wenye lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kukuza uwekezaji mkoani humo, Kairuki alipongeza mkakati wa mkoa kuandaa mwongozo kwani utakuwa dira kwa sekta za uwekezaji na biashara.

Aidha, amekiagiza Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) chenye dhamana ya kutangaza vivutio uwekezaji kutumia tovuti ya Mkoa wa Mara kuzitangaza fursa zote zilizopo mkoani humo ili kuchochea uwekezaji zaidi.

Alisema lengo la mkutano huo wa majadiliano na sekta binafsi ilikuwa ni kuibua na kubaini changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji ili kupata mapendekezo yatakayojenga mwelekeo wa pamoja katika kuzitumia fursa zilizopo kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Alisema Mkoa wa Mara una fursa nyingi katika sekta za uvuvi, kilimo cha pamba, miwa, kahawa, uzalishaji wa vifaranga, viwanda vya kuchakata samaki na nyinginezo nyingi zinazohitaji kubadilisha maisha ya watu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Manyanya alisema Mkoa wa Mara una nafasi kubwa ya kuanzisha viwanda vikiwemo vya mifuko ya ngozi kwani soko lake ni kubwa ndani na nje ya nchi.

Dk Kijaji alisema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini ikiwa ni pamoja na kupunguza utitiri wa kodi, tozo na ada mbalimbali ili kumrahisishia mfanyabiashara kufanya shughuli zake.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka mikoa 12 ifi kapo Septemba ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Musoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi