loader
Picha

‘Tumieni nishati ya chokaa mazao kurutubisha ardhi’

KATIBU Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Iringa anayeshughulikia masuala ya uchumi na uzalishaji, Eliya Mvanda amewahimiza wakulima kutumia nishati ya chokaa mazao ili kurutubisha ardhi iliyopoteza thamani yake.

Hatua ya matumizi ya Chokaa Mazao itasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali na hatimaye kuongeza tija kwa mkulima mmoja mmoja na hatimaye kwa taifa zima.

Mvanda aliyasema hayo jana Iringa wakati akizindua Mradi wa ‘Kuboresha Udhibiti wa Tindikali ya Udongo kwenye Ardhi ya Kilimo Tanzania’ (ECACLT).

Alisema mradi huu umekuja wakati mwafaka wakati serikali imeweka kipaumbele katika kuimarisha afya ya udongo hasa katika kubatilisha tindikali katika udongo.

Nishati hiyo inazalishwa na Kampuni ya Dodoma Cement kama mzalishaji wa Chokaa Mazao, ambayo katika kipindi cha 2020/21 inatarajia kusambaza bidhaa hiyo nchini ili kubatilisha tindikali katika udongo na kuleta tija kwenye kilimo.

Katibu Tawala huyo alisema kutokana na tafiti zilizofanywa na taasisi za kitaaluma na utafiti za TARI Uyole, SUA na za kimataifa, zimeonesha rutuba katika udongo kwenye baadhi ya maeneo ya Tanzania imepungua kutokana na kulimwa na kutifuliwa mara kwa mara bila kuwa na mikakati thabiti ya kuhuisha udongo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dodoma Cement, Charles Numbi alisema lengo ya kampuni hiyo kuzalisha tani 15,000 za Chokaa Mazao kwa mwaka kwa ajili ya kukidhi mahitaji katika mikoa ya Iringa, Rukwa, Katavi, Njombe na Ruvuma, ambayo imeathirika zaidi za tatizo la tindikali.

Alisema kampuni hiyo inashirikiana na Idara za Kilimo katika halmashauri za mikoa ya Iringa, Rukwa, Ruvuma, Njombe na Katavi na taasisi binafsi za ADP-Mbozi na RUCODIA.

Numbi alisema watawajengea uwezo wakulima na wauzaji wa pembejeo wa mikoa hiyo, kwa lengo la kuboresha uuzaji na usambazaji wa chokaa mazao kwa wakulima takribani 50,000 na ardhi ya kilimo isiyopungua hekta 20,000 katika mikoa hiyo.

Kampuni hiyo yenye makao yake makuu jijini Dodoma, imejikita katika uzalishaji na usambazaji wa Chokaa Mazao inayotumika kwa ajili ya kutibu udongo ulioathiriwa na tindikali kwa takribani miaka mitano sasa.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Iringa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi