loader
Picha

Tanzania kunufaika na miradi sita nishati Sadc

PAMOJA na changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Nishati katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ikiwemo kutokuwa na kituo rasmi cha nishati jadidifu cha kikanda, miradi mikubwa sita ya nishati ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Miradi hiyo inatekelezwa kwa hatua mbalimbali na Kituo cha Umahiri katika Uendelezaji wa Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati (SACREEE) kinachosubiri sahihi tatu kati ya 11 zinazohitajika kuwa na uhalali wa kisheria kutekeleza majukumu yake ya kisekta.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SACREEE, Kudakwashe Ndhlukula, alipozungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Wataalamu, Wakurugenzi na Makamishna wa Nishati ya SADC unaofanyika kwa siku nne kuanzia juzi, jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaohudhuriwa na wataalamu kutoka nchi 12 za SADC wa sekta ya nishati, ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Zena Said na utajadili pia Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia wa SADC.

“Miradi mingi inaweza kutekelezwa ikiwa tutakuwa na kituo cha nishati jadidifu kilicho na meno kisheria, inakwama kwasababu sahihi za nchi tatu wanachama zinategemea namna nchi husika zinavyoshughulikia mambo yake ya ndani. Wengine lazima wafikishe kwenye Bunge, wengine Baraza la Mawaziri na wengine wazirei mwenye dhamana tu anaweza kusaini ikatosha,” alisema Ndhlukula.

Alisema pamoja na kwamba SACREEE inakosa nguvu kisheria, lakini tayari inatekeleza miradi sita muhimu ya kimkakati ya nishati inayofadhiliwa na mashirika kadhaa ya kimataifa na nchi zilizoendelea washirika wa SADC. Kwa mujibu wa Ndhlukula, miradi hiyo ni Programu ya Ufanisi wa Nishati ya Viwandani (SIEEP) inayofadhiliwa na Serikali ya Austria kupitia Mkakati wa Viwanda wa jumuiya hiyo mwa mwaka 2015-2063 na wa kuwawezesha wajasiriamali kupata fursa, mitaji na kukua.

Mradi huo wa kuwezesha wajasiriamali ambao Tanzania inahusika unafadhiliwa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA) na tayari wajasiriamali 30 kutoka nchi wanachama watafanyiwa mafunzo hivi karibuni. Mwingine ni wa Utafiti unaolenga kutoa ujuzi kwa wataalamu wa SADC, upatikanaji wa vifaa na matokeo ya utafiti mbalimbali wa namna ya kutumia rasilimali za nchi wanachama kujitosheleza kwa nishati.

Mradi huu unafadhiliwa Serikali ya Uingereza kupitia Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID). “Mradi wa Utafiti unafanyika sambamba na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa katika sekta ya nishati, changamoto kubwa ni matumizi ya nishati itokanayo na maji.

Kama ujuavyo kuna majanga ya asili yanayoleta ukame, tunataka kuondoka huku na kuangalia eneo la upepo na nyuklia,” alisema Ndhlukula.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imenunua pikipiki saba zenye thamani ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi