loader
Picha

Mtanzania aingia 16 bora ubunifu Jumuiya Madola

TANZANIA imejipatia sifa kubwa baada ya kijana Salvatory Kessy kuingia kwenye orodha ya vijana wabunifu 16 kati ya 500 walioomba, wanaoshindania tuzo ya mwaka huu ya Jumuiya ya Madola, Machi 11 jijini London, Uingereza.

Kessy na wenzake wawili Adam Duma na Seraphin Kimaryo wameatamiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambacho kinasaidia vumbuzi na biashara mbalimbali zinazoanzishwa na wanafunzi na wakufunzi chuoni hapo kukua, kutengeneza ajira mpya, kukuza uchumi wa watu na nchi, pia kuitangaza Tanzania duniani kote.

Akizungumza na waandishi wa habari kupitia mtandao wa skype, Kessy aliyeko masomoni Austrlia alisema wameingia kwenye orodha hiyo kupitia mtandao wao wa SmartClass unalotumia teknolojia ya hali ya juu kuwaunganisha walimu na wanafunzi wanaotaka kujifunza mambo mbalimbali. Alisema kupitia mtandao huo mwalimu anaweza kumfundisha mwanafunzi kupitia njia ya mtandao au kwa kukutana nyumbani kwa mwanafunzi.

“Baada ya hapo kama mwalimu atakuwa ni mzuri tutamsajili kwenye mtandao wetu,” alisema.

Alisema mbali na ajira na kuwafundisha wanafunzi, kupitia ushiriki huo wanaleta sifa nzuri kwa taifa kwa upande wa teknolojia kwani wanajitahidi kukimbizana na mataifa mengine Afrika.

“Lengo letu ni kuhakikisha inakuwa ni kampuni ya kwanza ya kiafrika itakayosambaa Afrika na sehemu nyingine kama Asia ambao wanauhitaji mkubwa sana wa huduma ambayo tunaitoa. Nina uhakika nchi yetu itapata fedha za kigeni kupitia mtandao wetu wa SmartClass,” alisema.

Naye Mwanafunzi wa UDSM ambaye ni Ofisa Uendeshaji wa mtandao huo wa SmartClass, Adam Duma alisema walikuwa na wazo hilo mwaka juzi kisha mwaka jana walifika UDSM kwenye Kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali (UDIEC) hapo waliatamiwa mpaka wakaweza kuwafikia watu.

Alisema Februari 10, mwaka huu wameanza kutoa huduma hiyo nchini Kenya lengo lao likiwa ni kutatua tatizo la ajira pamoja na elimu kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu na kuishia mitaani. Alisema mtandao huo unagusa maisha ya watu wote kwani vijana wakijasili wanatumia elimu walizonazo kuwapa wengine na wale wenye uhitaji hutafuta walimu husika kupita huko.

“Kwa mwaka mmoja umegusa maisha ya walimu 5,000 kuwafikia wanafunzi 20,000. Kabla ya mwaka 2030 tunatamani kuwafikia watu milioni moja,” alisema.

Awali Makamu Mkurugenzi wa UDIEC, Dk Amelia Buriyo alisema UDSM ipo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa ubunifu wa vijana unakuzwa na kuchangia katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii ikiwemo ajira.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi