loader
Picha

Kocha Simba aipotezea Yanga

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck ameupotezea mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga unaotarajiwa kuchezwa Machi 8 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kujinasibu kwamba akili na nguvu zake ni mchezo unaokuja wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC.

Sven alitoa kali hiyo juzi kwenye mchezo ambao waliwang’oa Stand United Inyoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa mikwaju ya penalti 3-2 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam kwenye Uwanja wa Kambare, Shinyanga.

Alisema kuwapumzisha wachezaji wake wanaunda kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Stand sio kwamba alikuwa anajipanga kwa ajili ya Yanga, kwani lengo ni kushinda mchezo wai ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

“Nimetumia wachezaji wa kikosi cha pili kwa lengo la kuwapumzisha wachezaji wa kikosi cha kwanza kujipanga na michezo ya ligi kwakuwa ratiba yetu ni ngumu na mechi inayofuata tunacheza na KMC mchezo ambao utakuwa mgumu, lakini tunahitaji ushindi.

Nauchukulia mchezo dhidi ya KMC kwa umuhimu mkubwa kwani bado wanahitaji ushindi ingawa mashabiki wengi wanafikiria kwamba nimewapumzisha wachezaji wa kikosi cha kwanza na kutumia kikosi cha pili kwa lengo la kujipanga na mechi ya Machi 8 dhidi ya Yanga, hilo wala silifikirii, “ alisema Sven.

Sven alisema kwasasa hawezi kufikiria kuanza kuwapa mbinu wachezaji wake kwa ajili ya mchezo wa watani wa jadi, kwani sasa akili yake iko katika mchezo dhidi ya KMC na Azam, ambayo itafanyika kabla ya ule wa Yanga.

Sven kwenye mchezo dhidi ya Stand aliwapanga baadhi ya wachezaji wa kikosi cha pili, akiwemo Chiza Kichuya, Michael Dadiel, Beno Kakolanya, Haruna Shamte, Tairon Santos, Kennedy Juma, Sharaf Shiboub na Gerson Flagaa ambao mara nyingi wamekuwa wakitokea benchi.

Sven amewapongeza wachezaji wake kwa kazi nzuri waliyofanya kwa kupambana mwanzo mwisho na kufanikiwa kupata ushindi unaowafanya kujipanga wakisubiri kupangiwa mpinzani wa kucheza naye kwenye hatua inayofuata.

MSAJILI Msaidizi wa Vyama vya Michezo Jiji la Arusha, Benson ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi