loader
Picha

Balozi- Wachezaji wajitume

WANAMICHEZO wa Tanzania wametakiwa kupambana kwa bidii ili kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan 2020, imeelezwa.

Balozi wa Japan nchini Tanzania, Shinichi Goto ametoa wito huo jana katika ofisi za Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) alipokwenda kukabidhi fedha zilizochangwa na umoja wa kampuni za Japan zilizopo nchini.

Goto amesema wao watasaidia kambi ya maandalizi ya timu ya Tanzania baada ya wachezaji kufuzu, hivyo aliwataka wachezaji kuweka bidii katika mashindano ya kufuzu ili kufikia viwango vilivyowekwa na wao wataisaidia timu hiyo kwa maandalizi ya Olimpiki.

Amesema wako tayari kusaidia timu ya Tanzania itakayoshiriki Olimpiki 2020 na alisema wataongeza nguvu zaidi kuwaandaa wale walifuzu kwa michezo hiyo na kuwataka wachezaji kujituma zaidi.

Pia balozi huyo alisema kuwa pia amechukua jukumu la kuiandaa timu ya Tanzania itakayokwenda Tokyo kushiriki michezo hiyo ya Olimpiki Tokyo.

Makamu wa Rais wa TOC, Henry Tandau alisema kuwa wameomba sehemu mbalimbali kuomba fedha za maandalizi na kuna njia nyingi zinafanywa kwa ajili ya kukusanya fedha hizo.

Alisema umoja huo wa makampuni ya Japan umeahidi kutoa kiasi cha Dola za Marekani 1,000 huku akina mama wa Japan walipo nchini wamechanga fedha taslimu Sh 600,000 na Goto dola 50,000, ikiwa ni mchango wake binafsi, ambazo zilikabidhiwa jana.

Rais wa TOC, Gulam Rashid alisema kuwa kupitia ubalozi wa Japan, Tanzania imepata mualiko kutoka mji wa Nagai kupeleka wachezaji wa riadha na judo kwa ajili ya kujiandaa kwa mashindano ya kufuzu nchini Morocco kwa ajili ya judo.

Alisema riadha tayari kuna wanariadha wawili, Alphonce Simbu na Failuna Abdi huku wataangalia uwezekano wa kusaidia kwa ajili ya wanariadha wengine kushiriki mashindano mbalimbali ya kufuzu kwa Olimpiki.

Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi alisema kuwa baada ya mashindano ya ndondi ya ya kufuzu kanda ya Afrika na mabondia wote wanne wa Tanzania kudundwa, wanaangalia uwezekano wa kuwapeleka mabondia wawili katika mashindano ya dunia ya kufuzu Paris, Ufaransa Mei 13-20.

MSAJILI Msaidizi wa Vyama vya Michezo Jiji la Arusha, Benson ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi