loader
Picha

SMZ kugharamia Uchaguzi Mkuu

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itagharamia Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2020 kwa kutumia fedha zake zinazotokana na makusanyo ya kodi za ndani na haitategemea fedha za washirika wa maendeleo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, wakati akiwasilisha mwelekeo wa bajeti ya serikali pamoja na hali ya uchumi wa Zanzibar.

‘’Napenda kuwajulisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba, huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, ambapo wananchi hutumia fursa hiyo kuchagua viongozi wakuu wa kuwaongoza, tumejipanga kufanya uchaguzi kwa kutumia fedha zetu za ndani bila ya kutegemea washirika wa maendeleo,’’ amesema.

Hata hivyo, Balozi Ramia hakutaja kiwango cha fedha ambazo kimetengwa kwa ajili ya kugharamia uchaguzi huo. Mwaka huu wananchi watashiriki uchaguzi mkuu kuchagua Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani katika majimbo ya uchaguzi Unguja na Pemba.

“Kwa kawaida uchaguzi unatumia fedha nyingi ikiwa ni sehemu ya kutekeleza demokrasia, ambapo fedha hizo zitatolewa na serikali kupitia mapato yake yanayokusanywa nchini,” alisema.

Balozi Ramia aliwahakikishia wajumbe wa baraza hilo na wananchi kwamba, uchaguzi mkuu utafanyika katika mazingira yatakayozingatia demokrasia, huru na wazi.

Alisema maandalizi ya uchaguzi huo yameanza mapema, ikiwamo taasisi zinazoshughulika na uchaguzi, ikiwamo Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kujipanga vyema.

“Tayari harakati za kuelekea uchaguzi mkuu zimeanza, ikiwamo wananchi kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura pamoja na kufanya uhakiki wake.”

“Mchakato mwingine ni wananchi kupata vitambulisho vya Mzanzibari mkazi, ambavyo ni moja ya hatua muhimu ya kuelekea katika maandalizi ya uchaguzi huo kwa ufanisi mkubwa,” alisema.

SERIKALI imeshauriwa ione uwezekano wa kutenganisha mahabusu na wafungwa ili ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi