loader
Picha

Wawakilishi wapongeza utendaji wa Shein

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha Azimio la Kumpongeza Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, kwa utendaji wake wa miaka tisa, ambao umesaidia kuimarika amani na utulivu pamoja na kukuwa kwa uchumi na maendeleo ya wananchi.

Awali, Mwakilishi wa Mfenesini, Machano Othman Said pamoja na Mwakilishi wa Paje, Jaku Hashim Ayoub, waliwasilisha azimio hilo la kumpongeza Rais Shein kwa utendaji wake katika kipindi cha miaka tisa, huku maendeleo makubwa yakifikiwa katika sekta mbalimbali.

Said alisema katika kipindi cha miaka tisa, Rais Shein ameanzisha pensheni jamii kwa ajili ya wazee waliofikisha umri wa miaka 70, ambayo imeleta unafuu mkubwa kwa kundi hilo.

Alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika zinazotekeleza mpango wa pensheni jamii kwa ajili ya wazee waliofikisha umri wa miaka 70 na kutolewa bila ya ubaguzi.

Wakichangia azimio hilo, Mwakilishi wa Mtoni, Hussein Ibrahim Makungu, amesema Dk Shein ni kiongozi wa kupigiwa mfano, ambaye aliongoza Zanzibar katika kipindi kigumu cha Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Amesema serikali hiyo iliyowajumuisha wapinzani ilifanya kazi zake kwa maslahi ya taifa hadi pale wapinzani waliposhindwa kuingia katika serikali hiyo kutokana na kukataa kushiriki uchaguzi mkuu wa marudio mwaka 2011.

‘’Dk Shein ni Rais aliyefanya kazi kwa maslahi ya wananchi wa Unguja na Pemba kwa kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa ambayo hatimaye iliwashinda wenyewe wapinzani waliokuwa wakishinikiza tangu zamani,’’ alisema.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imenunua pikipiki saba zenye thamani ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi