loader
Picha

EU kutoa Euro mil 232 kudhibiti corona

UMOJA wa Ulaya (EU) umesema utatoa msaada wa euro milioni 232 kwa ajili kuongeza utayari, kuzuia na kudhibiti virusi vya corona. Msaada huo utasaidia katika kubaini na kugundua ugonjwa huo, utunzwaji wa watu walioambukizwa na kuzuia usienee zaidi.

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von de Leyen, alisema kuwa euro milioni 114 kati ya hizo zitaliwezesha Shirika la Afya Duniani (WHO) kuiandaa dunia katika hali ya utayari na kuitikia mpango huo, wakati euro milioni 100 zitatumika kwa utafiti unaohusiana na utambuzi, matibabu na kuzuia.

“Kama wagonjwa wanavyoendelea kuongezeka, afya ya umma ni kipaumbele chetu cha kwanza. Kama inaongeza utayari huko Ulaya, China au mahali pengine popote, jumuiya ya kimataifa lazima ifanye kazi kwa pamoja,”alisema Ursula.

Alisema sehemu nyingine ya fedha hizo, zitaelekezwa kwenye sekta tofauti. Zingine zitatolewa miezi ijayo.

Katika hatua nyingine, timu ya pamoja ya wataalamu kutoka China na WHO, imesema kuwa udhibiti wa homa inayosababishwa na virusi hivyo, umeanza kuwa na matokeo chanya, ikiwemo kuvidhibiti virusi hivyo kusambaa kutoka mtu hadi mtu.

Tathmini hiyo ilitolewa baada ya timu ya wataalamu 25, kufanya ziara ya siku tisa ya kikazi katika miji ya Beijing, Guangdong, Sichuan na Hubei.

Mbali na taarifa hiyo, imeelezwa kuwa China imewajibika vya kutosha katika kuilinda jumuiya ya kimataifa, kuzisaidia nchi nyingine kuchukua hatua za kuzuia na kudhibiti na kuwapatia uzoefu walionao kuhusu corona.

China imekuwa ikitoa taarifa kuhusu uelewa na usambazaji wa ugonjwa huo na hatari zake, hivyo nchi mbalimbali zimeshauri kuendelea kuchukua hatua za ufuatiliaji, ugunduzi, kuweka karantini na matibabu, pale zinapobaini kuwepo kwa ugonjwa huo.

foto
Mwandishi: BEIJING, China

1 Comments

  • avatar
    Ameir R.Msimbazy
    27/02/2020

    Kuna habari zinasambaa katika mitandao ya kijamii kwamba wachina wanaingia Tanzania kiasi cha 100/150 kila siku,na wafanyakazi wa KIA wanachukua namba zapasipotizao na anuani ya watakapo fikizia,kama hivyo ni kweli kwa nini serikali haichukui hatua kama nchi nyingine za kupiga marufuku wachichi wasiingie au kuwa karantini kwa wiki mbili au tatu kuhakikisha kwamba hawana hiyvo virusi? Na kama ni kweli wanaingia horera tumejitayarisha vipi na tunao uwezo huo? Nchi zote za Asia wamefunga mipaka wachichi wasiingie,kwanini tunakubali waingie halafu,wanajimwaga na watu wengine,hii kama kweli ni hatari ya hali ya JUU,naomba mtufahaishe,huu ni wakati wa sisi kuja kwetu kwa likizo na vijukuu,sasa itakua vipi? A.R.Msimbazy

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi