loader
Picha

Bila kibali huingizi nyama Tanzania

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewahakikishia wafugaji wa samaki nchini serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kuwawezesha wafugaji kufuga samaki.

Ameyasema hayo jana kwenye mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkutano huo umefanyika mjini Shinyanga, na mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah Kairuki.

"Kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, katika Ziwa Victoria tulikuwa na vizimba vya ufugaji wa samaki visivyozidi 50. Leo tuna vizimba zaidi ya 400 vya ufugaji wa samaki. Mwitikio ni mkubwa," amesema.

Amesema, baada ya jitihada za makusudi kufanyika, serikali haitaruhusu samaki kuingia nchini kwa sababu tuna uwezo kufuga wenyewe.

Amesema kwa upande wa Ziwa Victoria, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepata fedha nyingi kwa watu wenye lengo la kufuga samaki na kwa kuwa soko lipo la uhakika, ndiyo maana watu wengi wameingia katika ufugaji na uvuvi.

"Tumeweka mazingira mazuri ya kuhakikisha Watanzania wanaoingia biashara za mifugo na uvuvi wanapata soko. Awali tulikuwa tunaagiza nyama nyingi nje lakini Serikali imefanya kazi kubwa na sasa hatuingizi nyama kutoka nje isipokuwa kwa kibali maalumu tu," amesema.

Ulega amesema fursa kubwa iliyopo sasa ni biashara ya kunenepesha mifugo na kupeleka kwenye viwanda vya nyama vilivyoanzishwa.

Waziri Angellah Kairuki alisema serikali itawaunga mkono wafanyabiashara nchini na kuwakumbusha kufuata sheria na kanuni zilizopo katika biashara na uwekezaji.

Aliwataka wanapokuwa na migogoro yoyote wasisite kuwasiliana na serikali ili kuitatua.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka mikoa 12 ifi kapo Septemba ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi