loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wachimbaji wadogo walalamikia gharama

WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu kijiji cha Nyaligongo, kata ya Mwakitolyo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamelalamikia gharama za juu za uendeshaji wa shughuli zao kutokana na ukosefu maji na nishati ya umeme.

Mwakilishi wachimbaji wadogo Nyaligongo, Hussein Rashid alisema hayo katika kikao cha ushauriano na wafanyabiashara wa Shinyanga. Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angella Kairuki ambaye alikuwa ameambatana na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Ndaki alisema katika maeneo yao kuna planti 100 na kila moja hutumia lita 600 za maji. Alisema wanatumia jenereta kwa saa 24. Alisema umeme umefika tangu Desemba mwaka jana lakini umeishia kijiji namba tano. “

Tunaishukuru serikali kuanzisha masoko na maeneo ya uyeyushaji lakini Kahama bado ipo shida ya ucheleweshaji. Ingawa kwenda Kahama ni kilomita 45 na mjini Shinyanga ni kilomita 100, tumeona ni nafuu kukimbilia huko bila kujali umbali,”alisema Ndaki.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack alisema mkoa huo unaongoza kwa madini ya almasi na dhahabu lakini wachimbaji hupata kero ambazo zimekuwa zikitatuliwa taratibu.

Naibu Waziri Nyongo alisema changamoto hizo amezisikia na atafika siku nyingine kuangalia kwa undani kabla ya kutoa maelekezo zaidi. Alisema changamoto sasa ni dhahabu kuuzwa nzima hali inayolikosesha taifa mapato. Alisema upo mchakato kuchakata dhahabu kuwa vito mbalimbali kama vile hereni, pete na mikufu.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya Chama ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi