loader
Picha

Serikali yampongeza mzawa anayeunda mabasi

SERIKALI imempongeza aliyeanzisha kiwanda cha kuunda bodi za mabasi, Jonas Nyagawa ikisema ni taswira ya Tanzania ya viwanda. Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa alisema jana Dar es Salaam kuwa, uthubutu wa Nyagawa unatekeleza kwa vitendo falsafa ya uchumi wa viwanda na kusisitiza kuwa serikali inajivunia hatua yake hiyo.

“Tunampongeza kwa uthubutu wake, aliamini katika ndoto zake na kafanikiwa. Kuwa na kiwanda cha basi ambacho hata namba ya usajili ya chasis yake inaonesha ni mali ya hapa hapa nchini ni jambo zuri,” alisema Bashungwa.

Alisema alifanya ziara katika kiwanda hicho na kuridhishwa na maendeleo yake. Aliagiza watendaji wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Mabibo kukitembelea kiwanda hicho.

Mkuu wa NIT, Profesa Zacharia Mganilwa na timu yake ilifika kiwandani hapo kujionea maendeleo ya kiwanda kutekeleza agizo hilo. Nyagawa anamiliki kiwanda cha kuunda bodi za mabasi cha BM Motors, Kibaha mkoani Pwani.

Alisema ndoto yake itatimia basi la kwanza litakapoingia barabarani siku chache zijazo. Alisema basi hilo litaingia barabarani baada ya kukamilika kwa taratibu ikiwemo ukaguzi wa NIT na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Alisema wazo la kuanzisha kiwanda hicho lilimjia baada ya kuona changamoto ya kununua mabasi yalyokwishaundwa kutoka nje ya nchi.

Alisema mbali na kukosa ubora unaohitajika kulingana na barabara za nchini, pia gharama zake za kununua mabasi ya nje huwa ni kubwa.

“Nilipata wazo hili miaka mitano iliyopita nikachukua mkopo benki na kuanzisha kiwanda ingawa ukweli ni kuwa hata benki sikuwaambia nina mpango kuanzisha kiwanda cha kuunda mabasi nikijua ingekuwa vigumu kupata mkopo,” alisema.

“Nashukuru wazo langu linaenda kutimia. Nilichotaka ni kuweka historia kuna mtanzania alianzisha kiwanda cha kuunda mabasi,” alisema.

Alisema ujenzi wa kiwanda hicho kwa Sh bilioni mbili, unatumia asilimia 45 za malighafi zinazozalishwa nchini na malighafi nyingine kutoka kampuni mbalimbali zilizo nje ya nchi.

Alisema anachosubiri ni kununua mtambo wake utakaokuwa ukikunja ‘chasis’ hapa hapa nchini, tofauti na sasa ambapo mabasi mawili yaliyo hatua za mwisho za matengenezo chasis zake zilikunjwa China zikiwa na namba za Tanzania.

Alisema ameshapata oda kwa wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanaotaka kununua mabasi hayo baada ya kupata taarifa za uwepo wa kiwanda hicho. Alisema mabasi hayo yatakapoanza kuzalishwa mataifa mengi yatapigana vikumbo kununua.

WATU 11 wamekamatwa katika mpaka wa Horohoro uliopo kati ya ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi