loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

California yatangaza hali ya hatari, kisa Corona

JIMBO la California nchini Marekani, limetangaza hali ya hatari baada ya kutangaza kifo cha mtu mmoja kilichotokana na maambukizi ya virusi vya corona. Idadi hiyo imefanya watu waliokufa kwa ugonjwa huo nchini Marekani kufikia 11.

Mwanamume mwenye umri wa miaka 71, aliyefariki katika hospitali jirani na Sacramento, alikuwa na hali mbaya kiafya na alikuwa ni abiria kwenye meli. Serikali imeendelea na kampeni ya kutaka wananchi wake wote wapimwe ili kuona idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo.

Mpaka sasa watu 150 nchini Marekani, wameripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19 kutoka majimbo 16 nchini humo. Aidha, imethibitishwa kuwa zaidi ya watu 92,000 duniani, wana virusi hivyo vya corona na kati yao zaidi ya 80,000 wanatokea China.

Zaidi ya watu 3,000 wamefariki dunia duniani kote, wengi wao wakitokea China, ulikozuka ugonjwa huo mara kwanza . Nchini Marekani, watu 10 kati ya 11 waliopoteza maisha kwa corona, wanatokea jiji la Washington.

Maambukizi pia yameripotiwa kusambaa kwenye majiji ya Texas na Nebraska. Mwishoni mwa wiki majiji ya Washington na Florida, yalitangaza hali ya hatari kutokana na uwepo wa virusi hivyo vya corona.

Inaaminika kuwa mtu aliyefariki dunia jijini California, aliathirika na virusi hivyo kupitia kwenye meli ya Grand Princess, iliyokuwa ikizunguka kutoka San Francisco kwenda Mexico mwezi uliopita.

Baada ya meli hiyo kutia nanga San Francisco Februari 21, mwaka huu, baadhi ya abiria walishuka na wengine walibakia na chombo hicho kikaendelea na safari yake hadi Hawaii. Grand Princess ni moja ya meli kubwa za kitalii. Abiria wake 62 walizuiliwa kwenye vyumba vyao kwa ajili ya kupimwa, kama wamepata maambukizi ya ugonjwa huo.

WAOKOAJI nchini Lebanon wanatafuta zaidi ya watu 100 waliokufa na ...

foto
Mwandishi: CALIFORNIA, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi