loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongereni wanawake kuchangia maendeleo ya nchi

LEO wanawake nchini wanaungana na wenzao duniani kote kuadhimisha Siku ya Wanamke Duniani.

Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na sherehe za kumbukumbu ya miaka 25 ya mkutano wa wanawake duniani uliofanyika Beijing, China kujadili maendeleo na changamoto za wanawake.

Katika mkutano huo wa Beijing, Tanzania iliwakilishwa na Balozi Getrude Mongella, Spika mstaafu wa Bunge la Afrika na mbunge na waziri wa zamani katika serikali ya awamu ya kwanza aliyekuwa Katibu.

Wanawake nchini wanaadhimisha siku hii muhimu katika muktadha wa maendeleo ya mwanamke duniani.

Tunaungana na wanawake wote nchini na duniani kote kuadhimisha siku hii tukithamini mchango mkubwa wa mwanamke tangu enzi za Adam na Hawa hadi leo kwa sababu wameonesha uwezo mkubwa wa kazi.

Wakati dunia ikiendelea kupita katika hatua mbalimbali za maendeleo ya sayansi na teknolojia, mageuzi na mabadiliko ya kisiasa, kisheria, demokrasia, maendeleo, kijamii na utamaduni, mwanamke hajaachwa.

Ni kwa msingi huo tunawiwa kuwapongeza wanawake wa Tanzania na kwingine duniani kwa kusimama kidete kutetea haki zao na za watoto wao, kwa maana ya raia wote wa dunia hii wakiamini katika usawa.

Ni matarajio yetu kuwa sherehe hizo za leo zitazidi kuwakumbusha mchango wao katika malezi ya jamii na hivyo kuendelea kujitoa zaidi na zaidi kuhakikisha jamii yetu na dunia nzima, inaisha mahali salama.

Kwa muda sasa, nchi nyingi duniani zimeendelea kupita katika vita ya wenyewe kwa wenyewe au kati ya nchi na kuathiri maisha ya maelfu kwa maelfu ya kina mama na watoto hivyo kuwepo umuhimu wa amani.

Ndio maana tunaomba wanaume hasa wanasiasa kuungana na kina mama kuhakikisha dunia inakuwa mahali salama kwa wanawake, watoto na hata wao kuishi na kujiletea maendeleo ya kiuchumi na jamii.

Hadi sasa wanawake wameonesha wana uwezo wa kushindana na wanaume katika nyanja mbalimbali ikiwemo kushika nafasi mbalimbali za kisiasa, utawala, kidini na maeneo mengine kama wakiwezeshwa.

Mkutano wa Beijing ulifungua fursa nyingi za kuwawezesha wanawake na Umoja wa Mataifa (UN) na taasisi zake za masuala ya kina mama na mengine zimeendelea kusimamia kuwaendeleza wanawake.

Ni kwa msingi huo tunaomba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kuendelea kuwapa wanawake, fursa mbalimbali za uongozi katika medani ya kisiasa na utawala ndani na nje ya serikali.

Tunampongeza Rais Magufuli kwa kuenzi wanawake kwa kuteua mgombea mwenza mwanamke, Samia Suluhu Hassan na kufanya nchi iwe na Makamu wa Rais mwanamke. Hongereni wanawake kwa mafanikio.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi