loader
Picha

Watanzania changamkieni fursa ya maharage Ubelgiji

WIKI iliyopita Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilitangaza fursa mpya kwa wakulima na wafanyabiashara nchini Tanzania kutoka Ubelgiji.

Katika fursa hiyo, Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji umepata soko kubwa la maharage machanga ya kijani, yanayojulikana kama haricots vertz (green thin beans) nchini Ubelgiji.

Inaelezwa kuwa katika mazungumzo na pande hizo mbili na kampuni husika, kampuni CBG-Charlier- Brabo Group ya nchini humo ilieleza kuwa iko tayari kununua kontena 180 hadi 200 za maharage hayo kila mwaka kutoka Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini humo, Jestas Nyamanga ndiyo aliyowezesha kupata soko hilo, baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni hiyo CBG-Charlier-Brabo Group inanunua maharage hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuyauza katika maduka makubwa ya Carrefour, Delhaize na Aldi za nchini Ubelgiji, Luxembourg na nchi nyingine za Ulaya.

Ni dhahiri kuwa kupatikana kwa soko hilo kubwa, kunatoa fursa kwa wakulima kuchangamkia kwa kulima kwa wingi, huku wakizingatia kanuni za afya na viwango stahiki kimataifa kwa lengo la kuhakikisha soko hilo halipotei.

Tanzania na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo, hususan wa aina hiyo ya maharage, ambayo tayari Tanzania inayauza nchini Uholanzi kuhakikisha hakuna wafanyabiashara wa mataifa ya nje, watakaofika na kununua maharage hayo kwa wakulima na kuyauza kwenye kampuni hiyo.

Ni vema mamlaka husika, kuwasaidia wakulima wa maharage hayo popote walipo au watakaoanza kulima, kuunda vikundi kisha kuuza moja kwa moja kwenye kampuni bila kuingiliwa na wafanyabiashara wababaishaji.

Wakati mamlaka za mazao ya kilimo zikihakikisha maharage hayo yanauzwa yakiwa yameongezwa thamani na kufungashwa kwa viwnago vya kimataifa, inaelezwa kuwa kampuni hiyo.

Pia imeonesha utayari wa kununua aina nyingine ya maharage, ijulikanayo kama “red kidney beans” na “chickpea” kwa kiwango cha kontena nane kila mwaka katika hatua za mwanzo.

Hatua hiyo ni kubwa kibiashara, kwani itasaidia taifa kupata fedha za kigeni na kusaidia nchi kuachana na uuzaji wa maharage ndani ya nchi au nchi jirani pekee.

Lakini, kwa kuwa imeonekana maharage hayo, yanapendwa katika nchi hiyo na zingine, ni vema sasa kuwe na mkakati wa wataalamu wa kilimo, kuelekeza wakulima yanapostawi zaidi na kutumia kanuni za kilimo hicho. Hatua hizo zitawezesha kukamata masoko ya maeneo mengine duniani.

Lakini ili watanzania wanufaike na fursa hiyo, inatakiwa kuwe na mikakati madhubuti ya kampuni hiyo, kuwafikia moja kwa moja wakulima na pasiwepo watu wa katikati, watakaonufaika na fursa hiyo.

Ubalozi wa Tanzania umetaka Watanzania kuchangamkia fursa hiyo nchini Ubelgiji, kwa kuwasiliana na kampuni hiyo kupitia tovuti yao ya www. cbg.be au Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

MAPAMBANO ya ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) yanaendelea duniani ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi