loader
Virusi Corona vipo nchi 11 Afrika

Virusi Corona vipo nchi 11 Afrika

NCHI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imekumbwa na maambukizi ya virusi vya corona na kufanya jumla ya nchi za Afrika zilizokumbwa na virusi hivyo, kufikia 11 sasa na huku kukiwa na jumla ya wagonjwa 107 na vifo viwili.

Wizara ya Afya nchini DRC imethibitisha kuwepo kwa kisa kimoja cha mtu aliyeambukizwa virusi hivyo vinavyosababisha homa ya mapafu.

Mamlaka za Afya nchini humo zimesema vipimo vinaonesha kuwa mtu huyu mwenye uraia wa DRC ameambukizwa virusi vya corona na aliingia nchini humo hivi karibuni akitokea kwenye makazi yake nchini Ufaransa.

Kutokana na kisa hicho, DRC inakuwa miongoni mwa nchi 11 ambazo zimethibitisha kukumbwa na maambukizi ya virusi hivyo barani Afrika.

Kwa mujibu wa tovuti ya worldometer www.worldometers.info/coronavirus/#countries), nchi nyingine za Afrika zilizokumbwa na maambukizi ya virusi vya corona ni Misri yenye wagonjwa 59, Algeria (20), Afrika Kusini (7), Tunisia (6), Morocco (3), Nigeria (2), Cameroon (2), Togo (1), Senegal (4) na Burkina Faso (2).

Kuthibitika kwa mgonjwa wa corona nchini DRC kunaifanya nchi hiyo kupitia katika kipindi kingine kigumu kutokana na kuathiriwa na ugonjwa wa ebola kwa muda mrefu licha ya maambukizi kuanza kupungua.

“Inasikitisha kusikia kwamba wakati DRC inakaribia kumaliza tatizo la ebola, kirusi kipya kinatishia afya za raia wake,” amesema Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dk Matshidiso Moeti.

Dk Moeti amesema hata hivyo juhudi zilizotumika wakati wa mlipuko wa ebola zinaweza kuisaidia nchi hiyo katika kukabiliana na virusi vya corona. Alisema WHO imo nchini humo kulisaidia taifa hilo kama linavyoendelea kuwasaidia katika kukabiliana na ebola.

Kwa mujibu wa worldometer, tangu kuzuka kwa virusi vya corona, jumla ya watu 119,284 waliambukizwa, wengine 66,582 walitibiwa na kupona na vifo ni 4,300, huku nchi 119 duniani zimekumbwa na maambukizi hayo mpaka sasa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/73dcdbdb8fad934c820d214ed0eca4ac.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: KINSHASA, DRC

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi