loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Putin apinga Rais kupunguziwa mamlaka

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amepinga mapendekezo ya kupunguza mamlaka ya urais na kuyakasimu kwa Baraza la Ushauri au Baraza la Usalama kwa madai kuwa kitendo hicho kitasababisha mpasuko katika jamii na kuwa na mamlaka mbili zenye nguvu.

“Kukasimu baadhi ya mamlaka muhimu kwa vyombo vingine au mamlaka zingine kama vile Baraza la Usalama au Baraza la Ushauri, ukiachilia mbali wale ambao hawakuchaguliwa moja kwa moja na wananchi, linaweza kuwa jambo baya sana, kwa mtazamo wangu, itakuwa hatari,”amesisitiza Putin.

Putin amesema kwamba mapendekezo hayo hayahusiani na demokrasia na badala yake yataigawa jamii kwa kuwa na mamlaka mbili hali inayoweza kusababisha matokeo hasi na zaidi sana matokeo hatari kwa mustakabali wa taifa na watu wake.

Alisema Urusi kwa sasa inahitaji kuwa na kiti cha urais chenye mamlaka na kuongeza kuwa hali ya sasa ya uchumi na usalama ni ushahidi hai kwa jambo hilo.

Kwa mujibu wa Putin, demokrasia katika baadhi ya mabunge ya Ulaya imesababisha kushindwa kuundwa kwa serikali kwa miaka mingi na kuongeza kuwa kwa Urusi jambo hilo haliwezekani na halikubaliki.

WAANDAMANAJI katika mji wa ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi