loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vyama visipinge vijiandae kwa uhakiki

MSAJILI wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema wiki ijayo ofisi yake itaanza kuhakiki vyama 19 vyenye usajili wa kudumu.

Anasema Dar es Salaam juzi mchakato huo hauna lengo la kuvifuta baadhi ya vyama kwani kifungu cha 19 (3) cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019 hakiruhusu msajili huyo kufuta chama kama muda uliobaki kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika hauzidi mwaka.

Badala yake, alihakikishia viongozi wa vyama kuwa uhakiki huo umelenga kukagua namna vyama vinavyoendeshwa kama taasisi na si chombo cha mtu binafsi kinyume cha sheria.

Tunaungana na viongozi wa vyama vya siasa nchini kukaribisha uhakiki huo tukiamini kuwa utasaidia ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuwa na kumbukumbu za uendeshaji wa vyama vya siasa kulingana na taratibu za sheria.

Tunasema hayo tukirejea ukweli kuwa, ni muda mrefu ofisi hiyo haijafanya uhakiki kama huo na kuacha baadhi ya vyama vikijiendesha kiholela.

Ni kwa msingi huo tunasema uamuzi huu wa msajili ni mzuri na umekuja wakati muafaka ambapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani Oktoba, 2020.

Ni matarajio yetu kuwa, baada ya viongozi wa vyama husika kueleweshwa vizuri na msajili kuhusu azma yake, watatoa ushirikiano mkubwa kuiwezesha ofisi yake kupata taarifa inazotaka.

Ni jambo la kushangaza baadhi ya viongozi wa vyama vikubwa kulalamikia uhakiki huo kuwa umelenga kuvifuta baadhi ya vyama kuelekea uchaguzi mkuu wakati wanajua uhakiki huo ni sehemu ya utekelezaji wa usimamizi wa vyama.

Tunaomba msajili aendelee kutimiza adhima yake, asimamie Sheria ya Vyama vya Siasa na matakwa yake ili kujenga demokrasia pana ilivyodhamiriwa kujengwa.

Si sahihi hata kidogo kusikia baadhi ya vyama kimuundo ni vyama vya wanachama lakini ukija katika usimamiaji na uendeshaji wake, vimebaki kuwa chombo cha viongozi binafsi na si taasisi.

Viongozi ambao wanaendesha vyama vya siasa kama chombo binafsi wanapaswa kuelewa zile zama za kufanya mambo watakavyo, zimeisha.

Badala yake, wanatakiwa warudi kwenye mstari wa kufuata sheria, kanuni na taratibu rasmi za uendeshaji vyama zinazosimamiwa na msajili huyo.

Ni matarajio yetu uhakiki huu utakapomalizika, msajili atatumia taarifa alizopata huko kufanya marekebisho kwenye maeneo yenye upungufu.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi