loader
Picha

Mzazi kuwa mfano bora wa kuigwa

MWINJILISTI kutoka Marekani Bill Graham amewahi kusema “Urithi pekee ambao mzazi anaweza kumwachia mtoto wake au wajukuu zake si fedha wala mali zote ambazo ulizichuma kipindi cha uhai wako bali ni kumwachia tabia nzuri na imani.”

Pia mwimbaji Stacia Tauscher alishawahi kusema tunatumia muda mwingi kuwaza kesho ya watoto wetu bila kuwaza leo yao.

Leo hii wazazi wengi wanatumia muda mwingi kuwaza kuweka malengo ya watoto wao kufika vyuo vikuu na maisha yao bora ya baadaye kusahau kupanda mbegu bora leo ambayo itaota apo badaye.

Mara nyingi tumekua tukijiona ni wazazi bora kwawatoto wetu kwa yale tunayowatendea kumbe sisi wenyewe tumekua watengenezaji wa virusi katika maisha ya watoto wetu, bila kuelewa ni lini hivyo virusi vitajitokeza katika maisha yao na kuanza kuwatafuna, tunashindwa kujua kuwa vitakapoanza kuwatafuna wahanga wakubwa tutakua ni sisi wenyewe nakuanza kumtafuta mchawi bila kujua mchawi wa maisha yao ni sisi wenyewe, kwa malezi yetu na mienendo ya maisha yetu katika familia

Ukikaa na kuangalia mienendo mingi ya watoto wengi na uharibifu wao mwingi chanzo ni malezi ya wazazi sisi wenyewe ni kiasi kidogo walimwengu wanachangia uharibifu wa watoto waliopo katika kizazi hiki.

Kuna mwandishi mmoja wa vitabu anayetambulika kwa jina la Myles Munroe alishaaawahi kusema “mtoto ni sawa na CD tupu ambayo inategemea wewe unataka kuweka kitu gani ndani yake kutokana na vile unavyopenda kusikia kutoka katika CD hiyo.”

Tunaweza tukajiuliza mtoto mmoja ambaye uko naye nyumbani kwako anakushinda kulea matokeo yake anakua na tabia mbaya tofauti tofauti, lakini mtoto huyo huyo unamchukua na kumpeleka shule unayoona wewe ina maadili, na shule hiyo imebeba watoto elfu moja inafanikiwa kugeuza tabia ya mwanao na kuwa tabia njema.

Ulishawahi kujiuliza wamewezaje kugeuza tabia ya mwanao katikati ya watoto elfu moja na wewe umeshindwaje kurekebisha tabia ya mtoto mmoja ambaye kila siku unamuona na umemzaa mwenyewe na kumkuza mwenyewe, ukitafakari utagundua kwamba wazazi tuna matatizo.

Tatizo letu wazazi wengi katika jamii hii ya kitanzania tumekua tukiiga malezi ya kizungu na malezi ambayo tunaiga sio kwamba tumeyaona katika mazingira yao bali ni kuangalia katika television,bila kujiuliza je mazingira yetu yanaruhusu kulea watoto kwa namna hii? na matokeo ya malezi haya mwisho wake nini? je yatamsaidia mtoto kuishi vyema nawanaomzunguka siku zake za mbeleni utagundua ni lah! Kuna siku niikaa na mama mmoja katika sherehe moja akawa akinieleza sifa nzuri ya shule fulani.

Akanieleza kwamba mwanawe alikua mwizi sana na akirudi toka kazini anakuta kaiba vitu vya watoto wenzake na kaweka chini ya uvungu wa kitanda,mara kaiba baiskeli mara michezo mbalimbali ya watoto wenzie.

Akanieleza baada ya kumpeleka hiyo shule mwanawe akabadilika tabia zote mbaya alizonazo na akawa mtoto bora sana. Sasa nikajiuliza wale walimu wamefanya nini?kugeuza tabia za mtoto huyu na yeye alishindwa nini baadaya maelezo yake yote nikagundua tatizo lililopo hapa ni huyu mzazi alimpenda sana huyu mtoto,makosa ya mtoto hayakumshtua kwa upendo wa kupitiliza aliokua nao mzazi huyu kwa mwanae.

Wazazi wengi tunachozingatia kwa watoto wetu ni ufaulu wa darasani bila kujali ufaulu mwingine ambao ni muhimu, ambao ni maisha yanamzunguka katika jami.,Jinsiya kushinda tamaa ya pesa jinsi ya kukwepa marafiki waaribifu na jinsi ya kuweza kujidhibiti kuingia katika mapenzi wangali wakiwa shule, lakini tunachoangalia ni nafasi ya ngapi anapata akiwa darasani,je anamudu vizuri lugha ya kiingereza basi akiwa na mafanikio katika hayo tunaona tumefanikiwa katika malezi yetu.Kumbe kuna zaidi ya hayo katika malezi ya watoto wetu.

Tabia mbaya ya wazazi wengi katika jamii yetu ni kuzungumza mambo mengi ya kiutu uzima mbele ya watoto, matokeo yake watoto wengi wanakua na umri mdogo lakini akili kama ya watu wazima.wanapokua wakizungumza wanashindwa kuchanganua kwa upesi kwamba wanayozungumza hayafai kuzungumza mbele ya watoto matokeo yake watoto wadogo wanavutika na maneno yao, na matokeo yake ndo mapenzi kabla ya wakati na mimba za utotoni.nilishawahi kutembelea familia moja nilikutana na mtoto mwenye umri wa miaka tisa alikua darasa la tano.aliomba simu yangu akidai anataka kucheza michezo iliyopo katika simu.

Hakugundua kama nimempa ile simu lakini namfuatilia ni game gani anacheza alifungua mchezo mmoja lakini haikuchukua dakika nyingi alifunga ule mchezo akahamia upande wa meseji akaanza kufungua meseji anasoma moja hadi nyingine nikajiuliza huyu mtoto anafanya uchunguzi gani? baadaye nikagundua wazazi wake kuna vitu wanaongea mbele yake ambavyo mtoto anataka kuvihakiki kupitia simu yangu.

Hii akili ya huyu mtoto imeharibiwa na wazazi wake na huu uharibifu hautaishia kwake hii ni sumu ambayo anakwenda kusambaza kwa watoto waliokaribu yake. Ifike kipindi wazazi tujue mtoto ni nani, anahitaji nini? na tujizuie vipi hasira zetu mbele za watoto na kuzuia hisia zetu tunapokua nao ili tusiendeleze uharibifu katika kizazi hiki cha utandawazi ambacho kila siku vinaibuka vitu vipya vya kuharibu kizazi chetu .

Pia tumekua tukiwaachia uhuru wa kuangalia television vipindi vyote vya katuni bila kujua wala kuzitizama kwanza hizokatuni ili kujua zimebeba maudhui gani. Isitoshe maisha yetu tunayoishi katika familia zetu hayafai kuigwa na watoto wetu kwa kuwa hayapendezi,wazazi sisi wenyewe hatutamani kuwa mfano wa kuigwa kwa watoto wetu kwa kuwa maisha yetu hayana radha katika jamii tunazoishi.

Lakini kwa wakati huohuo tunatamani watoto wetu wawe na tabia njema wafanane na watu tunaoamini kwamba ni bora kuliko sisi tuliowazaa na wakue waje kuwa mfano bora katika jamii.

Kwa asili mtoto anaishi maisha ya mzazi wake ama wazazi wake. maana wanasaikolojia wanasema kwamba mtoto asilimia 80 anajifunza kwa kuona kuliko kusikia.

Sasa kama sisi wazazi wenyewe maisha yetu yamejaa magomvi,matusi na kutoelewana je tunapanda nini katika maisha ya watoto wetu?Jibu ni tunatengeneza mabomu ambayo yatalipuka katika maisha yetu kwa wakati usiotarajiwa.

Tuhakikishe tunajivunia watoto wetu katika nyanja zote sio katika elimu tu. Sasa hii ni kutengeneza mama mbaya wa baadaye au baba mbaya wa baadaye kwa familia yake na kutengeneza kizazi cha theory laini practical ni sufuri hii haitatusaidia kupata furaha ya baadaye.tu Tukizingatia malezi mazuri ya watoto wetu.

UGONJWA wa Corona unaosababishwa na virusi vya ‘Covid 19’ ulianza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi