loader
Picha

Wabunge- Wanaodhalilisha watoto waadhibiwe

WABUNGE wa Bunge la Vijana wameitaka serikali kuwachukulia hatua kali wote wanaodhalilisha watoto kingono. Walisema hayo wakati wa kikao chao kilichoketi mjini Mombasa, Kenya.

Wabunge hao wakiongozwa na Sabina Chege ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Seneta wa Nairobi, Johnstone Sakaja walisema wale wote wanaowapa watoto wa kike mimba, washughulikiwe ipasavyo kwa mujibu wa sheria.

“Tunawajua watu wote wanaofanya vitendo hivi katika jamii yetu, tunatakiwa kutengeneza sheria ya kuwashughulikia. Wana biashara gani na wasichana hawa wadogo?”alihoji Chege.

Chege alihoji uamuzi wa Wizara ya Elimu wa kuunda kikosi kazi cha kufuatilia suala la watoto wa kike, kupewa mimba ili kuwatambua wote wanaojihusisha na mapenzi na watoto.

“Kuna ulazima gani wa kuunda kikosi kazi kwa ajili ya kuchunguza kadhia hii wakati wahusika wote tunawajua? Baadhi ya familia huamua kujadiliana na wahalifu hao ili kuwaficha wasijulikane, lazima tuje na sheria ngumu sana,” aliongeza Chege.

Sakaja alisema ni aibu kuona asilimia 30 ya watoto, wanapata mimba kabla ya kufikisha miaka 19. “Wote wanaofanya unyama huu ni lazima wakamatwe,” alisema Sakaja.

FOMU za wagombea wanne kati ya 10 katika nafasi ya ...

foto
Mwandishi: MOMBASA, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi