loader
Picha

Miradi rafiki wa mazingira kufunguliwa EAC

KAMPUNI ya Global Capital Investment (GCI) ya Kenya, imepanga kutumia kiasi cha shilingi za Kenya bilioni 22 katika miradi ya maendeleo, ambayo itakuwa rafiki mkubwa wa mazingira.

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, ilisema inatarajia kuwekeza katika miradi mikubwa ya nishati mbadala, kama vile nishati ya jua na nishati inayotengenezwa kwa kutumia mabaki ya bidhaa mbalimbali wakati wa kuchakata bidhaa hizo (biomass).

Uwekezaji huo unatarajiwa kufanywa katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo ni Tanzania, Kenya na Uganda.

“Lengo la kuanzisha vinu hivyo vya nishati mbadala ni kupambana na uzalishaji na ueneaji wa hewa chafu ya kaboni na kutoa elimu na mafunzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yamekuwa yakisababishwa na uharibifu wa mazingira kutoka katika sehemu mbalimbali duniani,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kampuni hiyo ilisema ina lengo la kubadilisha mkondo wa matumizi ya nishati ya umeme kutoka vyanzo vinavyoharibu mazingira hadi katika nishati jadidifu, hasa katika mataifa ya Kenya na Uganda.

Kwa uwekezaji huo, kampuni hiyo ilisema ina uhakika wa kuepuka kiwango kikubwa cha hewa ya kaboni inayoharibu mazingira.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, uzalishaji wa nishati hiyo kwa kutumia vyanzo hiyo, utaathiri uzalishaji wa hewa chafu kwa tani 42,000 kila mwaka.

FOMU za wagombea wanne kati ya 10 katika nafasi ya ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi