loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nadharia ya John Rawls katika maadili

Wiki iliyopita, tuliichambua nadharia ya John Locke kwa minajili ya kuona mambo mazuri ni yapi na mambo mabaya ni yapi kwa mujibu wa nadharia hii.

Upembuzi huu unaweza kutusaidia kuona ni kwa vipi nadharia ya John Locke inaweza kusaidia katika kuyatazama maadili ya utumishi wa umma kwa namna nyingine nzuri.

Katika toleo hili, tunaichambua nadharia ya John Rawls ya mwaka 1971 ambayo imejikita katika haki zinazotokana na ushiriki wa mtu kwenye jamii yake, ili tuweze kuchambua mambo mabaya na mazuri kwa kutumia nadharia hii kama kioo na hatimaye tuweze kupanua zaidi wigo katika kuyatazama maadili ya utumishi wa umma.

Kwa mujibu wa Fallis katika chapisho lake la mwaka 2007 lenye kichwa cha habari “Information Ethics for Twenty First Century Library Professionals”, nadharia ya John Rawls, imejikita katika wazo fikirika la makubaliano (fair agreement).

Wanaohusika na makubaliano hayo hawajui chochote kuhusu mambo yao kama elimu, nafasi na hadhi zao katika jamii (behind a veil of ignorance), kwa minajili ya kuepuka hali ya upendeleo katika maamuzi yao, kuhusu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujua ni sera ipi ya kutumia.

Katika nadharia hii, Blackorby, Bossert na Donaldson katika chapisho lao la mwaka 2002 lenye kichwa cha habari:

“Utilitarianism and the Theory of Justice”, wanaonesha bayana kuwa jamii inaweza kuchukuliwa kama jamii nzuri endapo jamii hiyo haina aina yoyote ya upendeleo (bias) katika kubainisha mambo mazuri ya jamii (social good), ambayo yanatakiwa kutumika katika kuorodhesha mambo ya kuchagua kwa kuzingatia umuhimu wake kwa lengo la kupata mambo bora zaidi.

Japokuwa katika nadharia hii watu hawajijui kwa maana ya nafasi na sifa zao, bado nadharia yenyewe inawataka wajue kuwa wana uwezo wa kuanzisha, kuyafanyia kazi na kufanya mapitio ya kuboresha mambo mazuri na uwezo wa kuanzisha, kuendeleza na kuyaishi mazingira ya haki.

Wilkinson katika chapisho lake la mwaka 2014 lijulikanalo kama “Principlism and the Ethics of Librarianship” anaonesha kuwa kwa mujibu wa nadharia ya John Rawls, jamii nzuri ni ile ambayo watu wake wana nafasi ya kupata haki zao za msingi na vilevile watu katika jamii husika wanahakikishiwa usawa katika kupata fursa muhimu huku watu wenye mazingira magumu zaidi wakihakikishiwa mambo mazuri zaidi (the greatest benefit).

Meyers katika chapisho lake la mwaka 2003 lijulikanalo kama “Appreciating W. D. Ross, On Duties and Consequences na Goss katika chapisho lake la mwaka 1996 lijulikanalo kama “A distinct public administration” wanasema kuwa kwa mtazamo wa nadharia ya John Rawls, mazuri ya jamii yanatakiwa kugawika kwa watu wote kwa namna ambayo itapunguza hali ya kutokuwaa na usawa (harmful inequalities).

Hata hivyo, katika uhalisia watu wanafahamu vizuri mambo kama sifa, nafasi na hadhi zao katika jamii na kwa maana hiyo watu wenye nafasi zao wana uwezekano mkubwa sana wa kusimamia mambo ambayo yanawanufaisha wao binafsi dhidi ya wale wenye mazingira magumu ndani ya jamii kitu ambacho ni kinyume kabisa na matakwa ya nadharia yenyewe.

Kwa jumla, nadharia ya John Rawls inawahamasisha watu katika jamii kufanya maamuzi mbalimbali kwa kuzingatia mambo ya msingi na kuepuka mambo kama upendeleo unaotokana na kufikiria nafasi, sifa na hadhi zao, kwa vile mambo hayo yanaweza kuathili ubora wa maamuzi hayo kwa minajili ya kuhakikisha kuwa hata wale walioko pembezoni wanafaidika na haki za msingi na kupata fursa zinazoweza kuwafanya wakanufaika na mambo mbalimbali katika jamii.

Endapo watumishi wa umma watazingatia nadharia hii na kuhakikisha kuwa mambo mazuri yanapewa kipaumbele katika maamuzi na utekelezaji bila kujali wao wenyewe watafaidikaje na maamuzi husika kulingana na sifa, nafasi na hadhi zao, kuna uwezekano mkubwa wa jamii husika kunufaika na mambo mengi mazuri kwa manufaa ya wote.

Vilevile, watumishi wa umma wakizingatia mazuri ya nadharia hii, wanakuwa na nafasi nzuri sana ya kufanya tathimini nzuri na zenye uhakika juu ya seraka zilizopo, mfumo wa sheria pamoja na utekelelezaji wa miradi mbalimbali, ili kuona kama mambo hayo yanaweza kuwa mazuri kwa jamii nzima, hususan watu wa pembezoni kabisa au hapana.

Zaidi ya yote nadharia hii inaweza kabisa kuwa msingi mzuri wa kutetea sera mbalimbali, mifumo ya sheria na utekelezaji wa miradi ambyao ilianzishwa kwa kuzingatia maslahi ya umma, badala ya maslahi ya watu wachache wenye nafasi au hadhi kubwa katika jamii.

WAHENGA wanasema panapofuka moshi panaficha moto; ...

foto
Mwandishi: Dk Alfred Nchimbi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi