loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jina Babati linatokana na neno ‘baba yangu’

BABATI ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Manyara ni mji ambao upo umbali wa kilomita 172 kusinimwa Jiji la Arusha.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya ya Babati ilikuwa 303,013. Kihistoria asili ya jina Babati lilianzia mwaka 1918 wakati wa ujenzi wa barabara iliyokuwa ikipitia katika eneo ambalo leo kuna mji wa Babati.

Masimulizi yanaonesha kwamba wakati wa ujenzi wa barabara hiyo kulikuwa na msimamizi mmoja Mjerumani wa waafrika waliokuwa wanafanyakazi ya ujenzi huo wa barabara.

Mzungu huyo alimwona kijana mmoja wa kiume wa kabila la Gorowa (Kabila linalofanana na Wairaqw kwa kuzungumza) akiwa nje ya kibanda cha nyumba na pembeni yake walikuwepo wazee wawili wa kiume wakiwa katika mazungumzo. Mjerumani huyo akamsogelea yule kijana na kumuuliza jina la kijiji kile hicho ambacho leo ni mji wa Babati.

Yule kijana hakuelewa lugha ya Kijerumani na hivyo akadhani mzungu yule alikuwa anamuuliza kuhusu wale wazee wawili ni yupi baba yake kwa sababu pia kulikuwa na suala la kuwaajiri vijana kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Yaani akajua anaulizwa baba yako ni nani kati ya wale wawili. Yule kijana akajibu kwa Kigorowa akamtazama mzee mmoja kati ya wale wawili ambaye ni baba yake mzazi na kumjibu yule mzungu “Baba-ti” ikimaanisha ya kwamba huyu hapo ndiye ‘baba yangu’.

Mara moja yule Mjerumani akaandika katika kitabu cha kumbukumbu kwamba mahala sasa wanapofanyia kazi ni ‘Babati’ jina linaloendelea hadi leo.

Katika lugha ya Kigorowa mtu akitaka kusema huyu ni baba anasema ‘baba -ti’. Hii ni kwa mujibu akaunti ya Facebook ya Wakongwe wa Sumbawanga. Wewe unasemaje kuhusu asili ya jina hilo. Wasiliana na mhariri.

KATIKA jumla ya klabu 20 za Ligi Kuu England (EPL) ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi