loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EU wafanya mkutano kwa video hofu ya corona

VIONGOZI wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU), wamefanya mkutano wa kilele kwa njia ya video na kupitisha hatua kadhaa, kama vile kuweka vizuizi vya kuingia kwa watu kutoka nje ya Umoja huo ili kukabiliana na homa ya virusi vya corona (COVID-19.)

Mkutano huo uliofanyika jana, uliamua kuridhia pendekezo la Tume ya Ulaya, kuweka vizuizi vya kuingia kwa watu kutoka nje wa EU kwa kipindi cha awali cha siku 30. Katika kipindi hicho Umoja huo utahakikisha usambazaji na usafirishaji wa dawa, chakula na bidhaa kwa raia wa Umoja huo.

Aidha, mkutano huo ulikubali hatua zilizopendekezwa na Tume ya Ulaya, kuzuia kuuza vifaa tiba nje. Kampuni zitakazouza vifaa tiba kama vile barakoa, kwa kanda nyingine, lazima zipate idhini ya serikali ya nchi wanachama wa Umoja huo.

WAANDAMANAJI katika mji wa ...

foto
Mwandishi: LONDON, Uingereza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi