loader
Picha

Watoza ushuru maegesho magari Mwanza ni kero

WAFANYAKAZI wa kampuni za utozaji ushuru katika jiji la Mwanza, wamekuwa kero kubwa kwa sasa kwa baadhi ya wamiliki na madereva wa magari binafsi.

Wamejikita zaidi katika kuvizia magari, yanayoegeshwa sehemu zisizo na alama za vizuizi na kuwatoza madereva faini za fedha, kuliko kutoa maelekezo na kukusanya tozo kwenye maeneo husika.

Wanachofanya ni kukaa kwenye vichochoro na valanda za majengo, kuvizia wanaoegesha magari pembeni mwa barabara na mbele ya maduka.

Mtego wao huo umekuwa ukiwanasa madereva wa magari binafsi, wanaolazimika kuegesha magari na kushuka kupata mahitaji ya dharura yakiwamo ya ununuzi wa dawa kwa ajili ya wagonjwa.

Kitendo cha dereva kutelemka kwenda kutafuta mahitaji yake, hutoa mwanya kwa watoza ushuru wa maegesho, kufunga komeo maalumu kwenye tairi za gari husika, kisha kuondoka eneo hilo.

Cha kushangaza zaidi wanafunga magari hata kwenye maeneo yasiyo na vibao vya alama wala matangazo ya kuzuia maegesho.

Kero kubwa inakuwa pale dereva wa gari husika anaporudi na kukuta gari lake limefungwa komeo, huku wafungaji wakiwa hawapo na bila kuacha namba simu zao.

Hali hiyo husababisha dereva kuchanganyikiwa na kulazimika kusubiri kwa muda mrefu mpaka wafugaji wanapojisikia kurudi na kumtoza faini ya Sh 50,000. Kimsingi, sipingi suala la utozaji ushuru wa maegesho maeneo ya mijini maana ni mpango wa kuiingizia serikali mapato.

Lakini kero iliyopo ni uviziaji magari katika maeneo yasiyo na maelekezo yoyote na kutoza wahusika faini, bila kujali dharura iliyowalazimu kuegesha.

Inafahamika wazi kwamba mpango wa utozaji ushuru wa magesho ya magari, unalenga maeneo yaliyotengwa kwa ajili hiyo yenye michoro na ulinzi maalumu, si kila sehemu. Sambamba na hilo, watozaji ushuru huo wana wajibu wa kuelimisha na kuelekeza madereva wa magari kuhusu taratibu za uegeshaji usiokuwa na bughudha kwa watumiaji wengine wa barabara mijini.

Kwa mantiki hii, mamlaka husika zione umuhimu wa kuingilia kati suala hiliili kuwaondolea wamiliki na madereva wa magari binafsi kero ya kuviziwa na kutozwa faini holela.

Ninasisitiza kasumba ya kuvizia magari na kuwatoza wahusika faini kwenye maeneo yasiyo na alama wala matangazo ya kizuizi, ni kero iliyovuka mipaka jijini Mwanza.

Itoshe tu kuamini kwamba maofisa wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini Tanzania (Tarura), Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na askari wa usalama barabarani (trafiki) watashirikiana kutafuta haraka ufumbuzi wa kero hii.

TANGU kuingia nchini kwa mgonjwa wa kwanza aliyethibitika kuwa na ...

foto
Mwandishi: Christopher Gamaina

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi