loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake wana nafasi ya kuzuia na kumaliza Corona

UGONJWA wa Corona unaosababishwa na virusi vya ‘Covid 19’ ulianza kusikika kwa mara ya mwaka mwishoni mwa mwaka jana nchini China kwa kuambukiza watu kadhaa lakini baada ya muda ugonjwa huu ulisambaa kwa kasi na kusababisha nchi hiyo kusimama kwa muda.

Kutokana na kuathirika kwa kiasi kikubwa, nchi mbalimbali zilianza kuona athari ya ugonjwa huo ikiwemo Tanzania kwa baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kuingiza bidhaa, ambazo zilianza kuadimika na akiba zilizokuwepo madukani zilianza kupandishwa bei na mwisho kuadimika.

Kutokana na hilo, hapa Tanzania macho na masikio yalielekezwa kwa watanzania waliopo nchini China hususan wanafunzi waliokuwa katika mji wa Wuhan ulioathirika kwa kiasi kikubwa ,lakini Mungu ni mwema mpaka sasa China ikiwa haaina maambukizi mapya hakuna Mtanzania aliyepata ugonjwa huo .

Wakieleza mafanikio ya kutoambukizwa ugonjwa huo walisema ni kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya, kutokaa katika misongamano ya watu pamoja na kumuomba Mungu hivyo kupitia hili wanawake wanaweza kuonesha uwezo wao wa kulinda familia na taifa kwa ujumla.

Wanawake ni wakati wenu kusisitiza na kuelimisha familia zenu juu ya kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ikiwemo kuepuka misongamano ,kutulia nyumbani kama huna sababu ya kutoka na kubwa zaidi kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na kutumia vitakasa mikono kama una uwezo navyo.

Hakuna masihara wala mizaa katika hili, ugonjwa wa korona umeingia nchini na hususan katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha pamoja na Visiwa vya Zanzibar ambapo tayari kuna wagonjwa wamebainika pamoja na wengine zaidi ya 100 wakifuatiliwa, hivyo ni vema kuchukua hatua kuhakikisha tunalinda afya zetu.

Wanawake ni viongozi wa familia na ili kuhakikisha familia inakuwa salama ni vema kuzingatia maelekezo ya wataalamu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nje ya nyumba kuna maji na sabuni ili kila anayetoka nje nyumba na hata mgeni kanawe mikono kabla ya kuingia.

Pia kwa wanaoendelea na shughuli mbalimbali wahakikishe kila wanapoingia na kutoka wananawa mikono na kupata vitakasa mikono kama watakutana navyo hiyo itasaidia kufanya ugonjwa huo kuisha mapema na shughuli mbalimbali za maendeleo kuendelea ikiwemo watoto kurudi shule kwa ajili ya masomo.

Ni vema kutambua kuwa lengo la serikali kuwarejesha watoto nyumbani ni kusaidia kuepuka misongamano ambayo ni njia kubwa ya ugonjwa huo kuambukizwa hivyo wakiwa nyumbani ni vizuri wanaokuwepo wahakikishe watoto wanashinda nyumbani wakijisomea na siyo kuwaacha wakiangalia luninga kwani katika masomo muda huo wa siku 30 ni mkubwa sana.

Ni hatari kuacha watoto nyumbani wakizurura mitaani kwani wanaweza kupata ugonjwa na kuwaambukiza waliopo nyumbani, na kitendo cha kurudi nyumbani ikawa bure kwani madhara huwa ni makubwa wengi wakiambukizwa. Vile vile ni vizuri kudhibiti wageni wanaofika katika nyumba zetu bila sababu huku elimu ikiendelea kutolewa kwa wanafamilia wakiwemo wasaidizi wa nyumbani kuwa ugonjwa huo ni hatari kwa maisha, kiuchumi na kijamii hivyo lazima kila mmoja achukue hatua.

Katika kuhakikisha miili ya familia inakuwa na kinga ya kutosha, ni vema wanawake wakafuata na kusimamia ushauri wa madaktari na wataalamu wa afya lakini kubwa kutumia vyakula, matunda yenye mlo kamili ili kuimarisha kinga za mwili na kujikinga na ugonjwa huo. Lakini pia ni vema wanawake wakatumia muda kupata taarifa kamili kupitia vyombo vya habari makini na vile vya kuaminika na siyo kuchukua habari za mitandaoni na kuanza kuzisambaza na kuongeza hofu katika jamii pamoja na mizaha katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Raia yangu kwa kila mwanamke katika gamilia kuchukua hatua ya kuismamia hatua za usafi kwa kuanzia na usafi wa mikono na kuhakikisha wanafamilia wanatulia nyumbani kama hawana sababu ya kutoka nje ya nyumbani itasaidia kudhibiti maambukizi kwani watoto, vijana waliokuwa shule na vyuoni wamerejea majumbani.

KATIKA jumla ya klabu 20 za Ligi Kuu England (EPL) ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi