loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki yajipanga kuokoa uchumi Uganda

BENKI Kuu ya Uganda (BoU) imetangaza hatua saba za kuokoa uchumi wa Uganda katika kipindi ambacho zinahitajika nguvu kubwa za kifedha kukabiliana na virusi hatari vya corona.

Ujio wa virusi vya corona umekuwa hatari kwa uchumi wa nchi nyingi duniani kutokana na nguvu kubwa ya kiuchumi inayohitajika katika kupambana na virusi hivyo.

Fedha nyingi katika nchi mbalimbali zimekuwa zikitumika kupambana na virusi hivyo kuanzia ueneaji wake hadi kutafuta kinga pamoja na tiba. Hatua hizo kwa mujibu wa benki hiyo ni katika kushusha gharama ya fedha katika ulingo wa biashara na pia katika benki za kibiashara.

Miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa benki zote nchini Uganda zinaendelea kufanya shughuli zake bila kikwazo chochote hasa wakati huu ambao nchi mbalimbali zinasumbuliwa na ugonjwa wa COVID- 19.

Hatua ya pili ni kuhakikisha kuwa kila benki au taasisi ya fedha ambayo ipo chini ya usimamizi wa Benki Kuu inahakikisha usalama wa wateja wao, ikiwa ni pamoja na kila mfanyakazi wa taasisi hizo.

Hatua ya tatu ni kushiriki katika soko la kubadilishia fedha ili kuwa katika nafasi nzuri ya kutatua changamoto zitakazojitokeza kwa haraka hasa katika soko la fedha la dunia.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Uganda, hatua ya nne ni kubuni njia bora ambayo kwa kiasi kikubwa itapunguza matatizo katika soko hasa ikitokea kukiwa na uhaba wa mikopo katika benki mbalimbali.

Hatua ya tano ni kutoa msamaha wa angalau mwaka mmoja kwa taasisi za fedha zinazosimamiwa na BoU. Vilevile kuendelea kushirikisha taasisi za simu na baadhi ya benki ili kushusha tozo mbalimbali.

SERIKALI imesema nchi ina chakula cha kutosha, lakini kuna uwezekano ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi