loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Corona yapandisha bei ya mchele

WAKATI serikali ikitoa tahadhari ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona, tayari bei za bidhaa ukiwemo mchele zimepanda na kuanza kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonesha kwamba bei ya mchele imepanda na kufikia Sh 55,000 kwa gunia la kilo 50 badala ya bei ya zamani Sh 42,000.

Pia bei ya bidhaa nyingine ambazo zimepanda kimya kimya katika kipindi hiki cha tahadhari ya ugonjwa wa corona ni sukari pamoja na unga wa ngano.

Mmiliki wa duka la Mikungu, Ali Issa alikiri kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali muhimu za chakula katika kipindi hii cha tahadhari ya ugonjwa wa corona.

“Ni kweli bidhaa za vyakula zimepanda hapa ikiwemo mchele kwa tahadhari ya ugonjwa wa corona,” alisema.

Wizara ya Biashara na Viwanda imetoa onyo kwa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei ya bidhaa muhimu za vyakula na kusema hakuna sababu ya kufanya hivyo huku ikiwepo akiba ya kutosha ya chakula.

Waziri wa Biashara na Viwanda, Balozi Amina Salum Ali akizungumza na waandishi wa habari alisema takwimu zilizokusanywa na wafanyabiashara zinaonesha kwamba kuanzia Machi 17 mpaka Machi 20, bidhaa za mchele zilizokuwepo katika soko ni jumla ya tani 25,283,wakati sukari ni tani 11,750 na unga wa ngano ni tani 5,380. Alifafanua na kusema wastani wa matumizi ya mchele kwa mwezi ni tani 10,169,wakati sukari tani 3,000 pamoja na unga wa ngano 3,679.

“Napenda kuwajulisha kwamba bidhaa za vyakula zipo za kutosha, nyingine zikisubiri kushushwa katika bandari ya Malindi, kuna mchele tani 6,000 pamoja na sukari tani 760,” alisema.

Alisema tayari ametoa maagizo kwa taasisi husika ikiwemo uongozi wa Shirika la Bandari kuharakisha kushushwa kwa bidhaa hizo ili ziweze kuingia sokoni.

“Kwa ufupi upo uhakika wa chakula katika kipindi cha miezi sita sasa na hakuna sababu ya wafanyabiashara kupandisha bidhaa hizo bila ya sababu za msingi,” alisema.

Pia kwa upande wa bidhaa za mazao ya kilimo alisema uzalishaji wa vyakula umeongezeka kwa kiwango kikubwa na hakuna wasiwasi wa uhaba.

SERIKALI imesema nchi ina chakula cha kutosha, lakini kuna uwezekano ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi