loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Singapore yatoa dola 500,000 kukabili corona

SERIKALI ya Singapore imesema itachangia Dola za Marekani 500,000 kulisaidia Shirika la Afya Duniani (WHO). Fedha hizo zitatumika katika mkakati wa shirika hilo kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine.

Hayo yamo kwenye taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari ya Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Afya za nchi hiyo.

Taarifa hiyo ilisema mchango huo, unatokana na mwito wa Umoja wa Mataifa (UN) na WHO katika kupambana na virusi hivyo. Ilisema Singapore imeguswa mno na kuenea kwa virusi vya COVID-19 pamoja na athari zake kwa afya ya umma, jamii na uchumi na vifo vilivyotokea.

“Singapore itaendelea kufanya kazi kwa karibu na WHO na UN kuona namna bora tunayoweza kuchangia katika juhudi zinazoendelea,” zilisema wizara hizo katika taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Uganda imethibitisha kuwa na wagonjwa wanane wapya wa virusi vya corona, hivyo kufanya idadi ya wagonjwa kufikia tisa.

Waziri wa Afya wa Uganda, Dk Jane Aceng, alisema wagonjwa wote wapya ni raia wa Uganda waliokuwa safarini kutoka Dubai.

Wagonjwa sita kati ya wanane waligundulika baada ya kufika katika Kiwanja cha Ndege cha Entebbe. Wawili walipatikana katika maeneo yaliyotengwa kwa karantini binafsi.

“Wagonjwa wanane wa corona ni Waganda ambao walikuwa safarini kutokea Dubai, Falme za Kiarabu, wawili waligundulika Machi 20 na wengine sita Machi 22 wakiwa wasafiri wa mashirika ya ndege ya Emirates na Ethiopia,” alisema Aceng.

Alitoa mwito kwa wote waliosafiri kwenda Dubai hivi karibuni, kujitokeza ili wafanyiwe uchunguzi wa kiafya.

Kwa mujibu wa Dk Aceng, mpaka sasa wasafiri 2,661 wakiwemo Waganda, waliainishwa kama washukiwa wa maambukizi ya corona na kuwekwa karantini binafsi au karantini za kitaasisi. Kati ya hao, 1,356 wanafuatiliwa, 774 wako karantini za kitaasisi na 582 wako katika karantini binafsi.

WAANDAMANAJI katika mji wa ...

foto
Mwandishi: SINGAPORE, Singapore

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi