loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SMZ kutathmini uchumi baada ya corona

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kutathmini hali ya uchumi katika miradi yake na utalii kutokana na tishio la ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia alisema hayo alipofanya ziara kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na SMZ.

Miradi iliyotembelewa na Balozi Ramia ni ujenzi wa nyumba za maendeleo ya makazi ya wananchi Kwahani mkoa wa mjini magharibi Unguja na ujenzi wa jengo la Mahakama kuu ya Zanzibar Tunguu mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema serikali itahakikisha miradi hiyo inatekelezwa na kumalizika kwa wakati licha ya kuwepo hofu ya corona na uhaba wa mchanga.

Kwa mujibu wa Balozi Ramia tathmini ni muhimu kufanyika kusaidia kujua athari zilizopatikana kipindi cha corona ambapo mambo mengi yamesitishwa kufanyika.

Mhandisi mradi wa ujenzi makazi ya wananchi Kwahani, Emmanuel Mushi alisema ujenzi huo ulioanza Oktoba 2 mwaka jana unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba mwaka huu.

Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo alisema utalii ni kati ya sekta iliyoathirika kutokana na hoteli nyingi zinazopata watalii wengi Italia kufungwa. Uchumi wa Zanzibar kwa asilimia 27 unategemea sekta ya utalii huku asilimia 80 ya fedha za kigeni zikitokana na sekta ya utalii.

SERIKALI imesema nchi ina chakula cha kutosha, lakini kuna uwezekano ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi