loader
Picha

Daktari ataja makundi hatarini kupata TB

MAKUNDI ya wazee, watoto na watu wenye magonjwa ya kurithi, yapo katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kutokana na miili yao kuwa na kinga dhaifu, ikilinganishwa na makundi mengine.

Kauli hiyo imetolewa na Dk Peres Lukango, ambaye ni Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma katika Jiji la Dodoma wakati wa mahojiano kwenye Kituo cha Afya cha Makole, ikiwa ni Siku ya Kifua Kikuu Duniani, ambayo huadhimishwa Machi 24 ya kila mwaka.

Dk Lukango amesema kuna dalili ambazo hujitokeza kwenye ugonjwa huo ikiwemo mgonjwa kukohoa mfululizo, inatakiwa mtu aonapo dalili hizo awahi kwenye kituo cha afya.

Amesema dalili za kawaida za maambukizi ya kifua kikuu kinacholeta madhara ni kikohozi sugu na kukohoa damu, kohozi, homa, kutokwa na jasho usiku, na kukonda.

Maambukizi ya viungo vingine husababisha dalili mbalimbali. Pia alisema njia za kitaalamu, huweza kugundua kama mtu ameambukizwa ugonjwa huo na kuanzishiwa matibabu.

Alisema Jiji lina mikakati mbalimbali ya kuwatafuta, kuwafikia, kuwachunguza watu wenye maambukizi ya ugonjwa huo. Wanaothibitika wameambukizwa kifua kikuu, wanatakiwa kuwahi kwenye huduma ya matibabu na kuhakikisha huduma hiyo imekamilika.

Dk Lukango alisema wamekuwa wakizunguka maeneo mbalimbali ya Jiji, kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa huo na imewasaidia kwa kiasi kikubwa kugunda wagonjwa ambao wameambukizwa.

Muuguzi katika Kituo cha Afya cha Makole, Phoibe Nhonya alisema wamekuwa wakihudumia wagonjwa wa kifua kikuu kwa kuwapa dawa, ambazo hutumia kwa miezi sita.

Rose Lema ambaye ni mhudumu wa afya ngazi ya jamii, alisema wamekuwa wakiwafuatilia wagonjwa, ambao wameanza tiba ili wasiache na kuhudhuria kliniki inavyotakiwa, kwani wakiacha dawa watakuwa na TB sugu. Kaulimbiu ya Siku ya Kifua Kikuu duniani ilikuwa, "Wakati ni huu, tuungananishe nguvu na kuwajibika katika mapambano ya kutokomeza kifua kikuu’’.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma imehamasisha uzalishaji wa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi