loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Elimu zaidi inahitajika kuhusu udhibiti wa corona

WAKATI mataifa mbalimbali duniani yakihangaika kupambana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona, bado idadi kubwa ya Watanzania inaonekana kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya Covid-19.

Covid-19 ni ugonjwa hatari, ambao Shirika la Afya Duniani (WHO) limeutangaza kuwa ni janga la kimataifa kutokana na namna unavyoambukiza kwa haraka na kuua idadi kubwa ya watu kwa muda mfupi.

Ugonjwa huo ulianzia nchini China katika jimbo la Wuhan, ambapo hadi jana China pekee ilikuwa na watu walioambukizwa corona 81,171, wagonjwa wapya 78, waliofariki kwa ugonjwa huo 3,277, vifo vipya saba na waliopona 73,159. Hata hivyo, kutokana na kasi ya kusambaa kwa virusi hivyo, kwa muda wa miezi mitatu, corona ilitua katika takribani nchi 188 ikiwemo Tanzania, ambayo hadi mwanzoni mwa wiki hii, ilikuwa na wagonjwa wa corona 12.

Aidha, nchi za Afrika Mashariki na zile zinazopakana na Tanzania nazo zilikumbwa na dhahama hiyo, ambapo Kenya nayo mpaka sasa ina wagonjwa 16, Uganda tisa, Rwanda 36 na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) 36. Kwa takwimu za jumla hadi jana mchana watu walioathirika na virusi vya corona duniani, walifikia 383,900, waliopoteza maisha 16,586 na waliopona kwa ugonjwa huo ni 102,536.

Ukweli ni kwamba hali ya maambukizi ya corona, bado ni tete duniani kote, si Tanzania pekee, kwani takwimu za maambukizi mapya ya jana pekee duniani, zinaneosha watu 5,118 waliambukizwa corona huku waliopoteza maisha wakifikia 79.

Kutokana na hali halisi, ndio maana serikali iliamua kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti maambukizi ya corona, kwa kufunga shule zote za awali, msingi na sekondari, vyuo vikuu na vya kati, kuzuia misongamano ikiwemo semina, mikutano, warsha na makongamano.

Aidha, juzi Rais John Magufuli alitangaza kuwaweka abiria wote wanaoingia nchini, wakitokea mataifa yaliyoathirika karantini kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe na kuzuia safari zote za nje kwa watumishi wa umma.

Hata hivyo, pamoja na hatua hizo kuchukuliwa, bado watanzania wengi kutokana na mienendo yao, wanaonekana kutokuwa makini na tahadhari za ugonjwa huo.

Huko mitaani hususani jijini Dar es Salaam, milundikano imeendelea kama kawaida hususani kwenye daladala. Takribani daladala zote zinajaza kupita kiasi, jambo linalozidi kuwaweka hatarini abiria hao, endapo kutakuwa na mtu mmoja tu mwenye maambukizi.

Pamoja na daladala, lakini mitaani bado wazazi wanawaachia hovyo watoto wao bila kuwapa elimu ya kutoshikana mikono au kukumbatiana pamoja na kunawa mikono.

Mitandaoni ndio kuna kero kubwa kutokana na watu wanavyoufanyia mzaha ugonjwa huo, ambao duniani kote hasa kwenye mataifa yaliyoathirika zaidi na kupoteza watu wengi wanaugwaya.

Ni vyema wale walioanza kuchukua hatua za kudhibiti maambukizi wakapongezwa, kama vile maduka ya dawa, baadhi ya ofisi na maduka makubwa.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi