loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongera JPM, watu wahame kwenye mafuriko

KATIKA gazeti hili jana, kulikuwa na habari kuwa mafuriko Kibiti Mkoa wa Pwani yameacha kaya 500 hoi, kwa kukosa makazi baada ya nyumba kusombwa na maji yaliyotokana na mafuriko.

Pia, katika vyombo vya habari mbalimbali nchini, kumekuwa na habari za viongozi wa serikali wa wilaya na mkoa wa Iringa, Mpanda mkoani Katavi na Chunya mkoani Mbeya, kushughulikia mafuriko au madaraja kukatika. Mafuriko na madaraja yamekatika kumetokana na mvua kubwa kunyesha maeneo mbalimbali na kuzidi uwezo wa ardhi, kufyonza maji ya mvua.

Matokeo yake maji hayo yamevunja madaraja kama Kiegeya barabara ya Morogoro- Dodoma, Chunya na mengineyo, huku yakiacha mamia ya watu wakikosa makazi baada ya maji kufurika.

Mafuriko hayo yamesababisha viongozi wa serikali, kuchukua hatua za kuagiza wananchi wote walioathirika kwa nyumba zao kubomoka na kukosa malazi na chakula, kuhama makazi. Mbali ya Kibiti, Rufiji na Iringa, kumekuwa na mafuriko maeneo mengine nchini kutokana na maeneo hayo kuwa oevu na kutofaa kwa kuishi.

Ni kutokana na ukweli huo, tunaunga mkono kauli za viongozi wa serikali katika maeneo yote, yaliyokumbwa na mafuriko au madaraja kuvunjika kwa sababu ya nguvu kubwa ya maji, kuwataka wakazi wake kuhama maeneo hayo. Pamoja na kuwa tunajua watu hao wamepoteza mali zao, zikiwemo nyumba na chakula, si busara kwa hali ilivyo kuendelea kuishi huko.

Ni vyema wazingatie ushauri na maelekezo ya viongozi wa serikali, kuhamia katika maeneo makavu yasiyotuama au kufurika muda wote. Kitendo cha kulazimisha kuendelea na maisha maeneo hatarishi, si cha kuachwa tu kiendelee.

Ni matarajio yetu kuwa wananchi wote, ambao wametakiwa na viongozi wa serikali kuhama na kutorejea kwenye makazi yao yaliyofurika maji, hawatakaa warudi mvua inyeshe au isinyeshe.

Mafuriko waliyopata yanatosha kuwa fundisho kubwa kwao, familia zao na pia kwa serikali kuhusu uchaguzi wa maeneo mazuri ya kuishi. Ikibidi sana maeneo hayo yabaki kwa ajili ya kilimo, lakini makazi yao wayahamishie katika maeneo mapya, waliyopewa na serikali sasa.

Kinyume chake itakuwa sawa na kusema watu hao na familia zao, wako tayari kukabiliana na mafuriko na athari zake, jambo ambalo si zuri. Kwa mara nyingine, tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kwa jinsi inavyojali maisha ya Watanzania.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi