loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mahakama yakataa ripoti kuwa kielelezo

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imekataa kupokea ripoti ya ukaguzi iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dk Laurence Shirima katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (Rahco) kwamba muhuri wa moto uliowekwa hausomeki.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Benhadard Tito, Mwanasheria wa Rahco, Emmanuel Massawe na mfanyabiashara ambaye pia ni Mwakilishi wa Kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.

Akisoma uamuzi huo mdogo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema amepitia hoja zilizowasilishwa na Wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo akiomba kielelezo hicho kipokelewe na hoja za Wakili Peter Kibatala na Jeremiah Ntobesya waliokuwa wakipinga kupokelewa kwa sababu kina mapungufu.

Simba alisema nyaraka iliyowasilishwa imegongwa muhuri wa moto ambao hausomeki, hivyo haijulikani nyaraka inatoka wapi kwani muhuri unatakiwa kugongwa kila kurasa lakini hata ulipogongwa hausomeki.

Alieleza kuwa shahidi alitambua nyaraka hiyo kwa sababu ya muhuri wa moto na kwamba ripoti hiyo ilikwenda kwao wakaigonga muhuri lakini hausomeki hivyo mahakama inakataa kielelezo hiki.

Ripoti hiyo ya ukaguzi ilikuwa ikionesha mchakato wa kuipitisha Kampuni ya Rothschild kama mshauri wa mradi wa uimarishaji wa Reli ya Kati. Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili Mosi, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa kesi hiyo. Hata hivyo, mshtakiwa Kanji hakuwepo mahakamani hapo kwani ni mgonjwa yuko Hospitali ya Temeke.

Washitakiwa wote watatu wanadaiwa katika nyakati tofauti kati ya Septemba Mosi, 2014 na Septemba 30, 2015 katika Mkoa wa Dar es Salaam wanadaiwa walikula njama ya kutenda makosa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Inadaiwa kuwa Februari 27, 2015, Tito katika ofisi za Rahco zilizoko wilayani Ilala, alitumia madaraka yake vibaya kwa kuipitisha Kampuni ya Rothschild kama mshauri wa mradi wa uimarishaji wa Reli ya Kati bila idhini ya Bodi ya zabuni ya Rahco hivyo kwenda kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi