loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wolper awagwaya wanaume

MWIGIZAJI wa fi lamu na mfanyabiashara, Jacqueline Wolper, amewaomba radhi wanaume baada ya kutangaza sifa za mwanamume anayetamani kuwa baba wa watoto na simu kumiminika.

Wolper aliandika kwenye ukurasa wa Instagram sifa za mwanamume anayetamani awe baba wa watoto wake pamoja na namba ya simu, lakini hali imegeuka tofauti na alivyofikiria kwani amekiri kupigiwa simu nyingi na kuhisi simu itapasuka.

“Naomba mnisamehe kwa sasa hadi corona ipite maana si kwa simu hizi hadi nahisi simu itapasuka,” aliandika Wolper.

Wolper alitaja vigezo vya mwanaume anayemtaka kuwa asiwe tajiri. Awe mchapakazi ajue kazi na asichague kazi, hata akimwambia leo anaenda Kariakoo Shimoni kuna kazi ya nyanya imetoka wakanunue, wapate pesa awe tayari.

“Awe ana hofu ya Mungu, asiwe anavuta sigara wala unga ila kilevi chochote ruksa,” alisema.

Aliongeza kuwa awe msafi muda wote asiwe na mtoto na umri miaka 30 na kuendelea, urefu, ufupi uzuri siyo tatizo na haijalishi ana kazi au hana, “tutapambana na kazi yangu mpaka tuwe matajiri,” aliandika.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi