loader
Picha

Diamond awabwaga Wizkid, Davido mtandaoni

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefanikiwa kuweka rekodi mpya katika mtandao wa Youtube akiwa na wafuasi milioni 9 na wanaolipia huduma yake mtandaoni (shitariki) milioni 3.29 tangu ajiunge kwenye mtandao huo Juni 12, 2011.

Katika mtandao huo anatumia kuchapisha picha mjongeo mbalimbali ikiwemo ‘behind the scene’ na matamasha yake anayoyafanya ndani na nje ya nchi na nyimbo zake na matukio yote yanayomhusu binafsi.

Katika akaunti yake ya Youtube, wimbo ambao umeangaliwa zaidi kuliko nyingine ni Yope Remix aliyoshirikishwa na msanii kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Innoss’B ambao umetazamwa na watu milioni 74 ukifuatiwa na wimbo wa Nana aliomshirikisha Mr Flavour kutoka Nigeria na wimbo wa tatu ni Inama aliomshirikisha Fally Ipupa kutoka DRC.

Mbali na nyimbo hizo kuonekana kufanya vizuri katika akaunti yake hiyo ya Youtube siku za hivi karibuni alitoa wimbo wa Jeje ambao umesaidia kusukuma akaunti hiyo na kufikisha watazamaji hao.

Diamond amewapiku msanii Davido, kwani wimbo wake uliotazamwa mara nyingi kwenye akaunti yake ya Youtube ni ‘Fall’ ambao umetazamwa na watu milioni 161 ukifuatiwa na ‘IF’ wenye watazamaji milioni 102, huku Wizkid wimbo aliomshirikisha Drake ‘Come Closer’ ukiwa na watazamaji milioni 89.

Baada ya Diamond kuwa na watazamaji 903,908,807 anafuatiwa na msanii kutoka nchini Afrika Kusini, Die Antwoord mwenye watazamaji 893,236,573 mbali ya kugawanyika kwa sasa wasanii kutoka Nigeria, P Square wakiwa na watazamaji 791,497,698.

Davido akifuatia mwenye watazamaji 544, 143,482 huku Tecno akiwa na watazamaji 543,152,870 na Wizkid mwenye watazamaji 444,814,179 lakini pia Sinach kutoka Nigeria akiwa na watazamaji 444,459,523, Burna Boy mwenye watazamaji 429,531,415, Kwa upande wa wasanii wa Kitanzania, Diamond anafuatiwa na Harmonize mwenye watazamaji 356,320,274.

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi