loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mitandao waonywa taarifa za uongo

BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRACCC), imeonya watumiaji wa mitandao ya kijamii kusambaza taarifa za uongo kuhusu maradhi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Katika tarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa baraza hilo Mary Shao (pichani) alisema watumiaji wengi wa mtandao wachukue taadhari kuacha kusambaza habari za uzushi kwenye mitandao na kuepuka mkono wa sheria.

Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandao, namba 14 ya mwaka 2015, kinasema: Kutoa taarifa za uongo mtandaoni adhabu yake ni faini isiyopungua Sh milini tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

“Watumiaji wa mitandao tunawahadharisha, kipindi hiki cha mlipuko wa corona, kuepuka kusambaza taarifa usiyo na uhakika nayo, mwenye mamlaka ya kuzungumzia ugonjwa huu ni Waziri Mkuu au Msemaji wa Serikali au Waziri mwenye dhamana,”alisema.

Alisema licha ya kuwepo kwa sheria ya makosa ya mtandao, usambazaji wa taarifa za uongo mitandaoni umeendelea kuwa changamoto sugu hususani kipindi hiki kumeibuka taarifa nyingi za kuongofya kuhusu ugonjwa huo.

Kauli ya TCCRA CCC imekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kukemea tabia ya watu kusambaza habari za uongo za kutishana kuhusu ugonjwa huo wa virusi vya corona na kuwataka watu kuacha mara moja kuzungumzia ugonjwa huo.

Hata hivyo, Shao alisema kutokana na kushamiri kwa taarifa hizo za uongo na uzushi mitandaoni, kitengo maalumu cha makosa ya mtandao kinaendelea kufanya doria mitandaoni ili kuwabaini wahusika hao na wengine wa makosa ya mtandao.

Alisema kuna kesi nyingi za watu kusambaza taarifa za uongo kwa makusudi na wengine bila kufahamu kuwa ni kosa kisheria.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi