loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Abbasi- Hakuna maambukizi mapya corona

SERIKALI imesema hakuna maambukizi mapya ya virusi vya corona nchini zaidi ya wagonjwa 12 waliothibitika kuambukizwa hapo awali.

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi.

Dk Abbasi alilieleza HabariLEO kuwa serikali kwa sasa inaendelea kuwahamasisha wananchi ili waepukane na misongamano na kujikinga kiafya.

Alisema serikali imeashaanza kutekeleza maelekezo ya Rais John Magufuli ya kumtaka kila msafiri kutoka nchi ambazo zina maambukizi mengi ya virusi vya corona, kutengwa kwa siku 14.

Lengo la hatua hiyo ni kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo kupitia wageni, wanaoingia hapa nchini kutoka nchi zingine.

Alipoulizwa juu ya idadi ya watu waliowekwa karantini mpaka sasa, Dk Abbasi alisema si rahisi kwa sasa kujua idadi yao, kwa sababu watu wanaingia nchini kupitia sehemu tofauti tofauti au vyombo tofauti tofauti, kama vile ndege, meli na mipaka.

Taarifa ya hivi karibuni ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imeeleza kuwa mpaka sasa watu waliokutwa na maambukizi ya virusi vya corona ni 12 na wanane kati yao ni Watanzania.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘worldometers’, mpaka jana duniani kote, kulikuwa na wagonjwa 425,959 wa homa ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona na vifo vilikuwa 18,957.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi