loader
Picha

DC- Mchina hana corona, alikuwa amelewa

MKUU wa Wilaya ya Mkinga, Yona Mark amesema Mchina aliyehisiwa kuwa na corona, aliyetaka kuingia nchini Tanzania kutoka Kenya kupitia mpaka wa Horohoro, hakuwa na corona, bali alikuwa amelewa.

Yona amebainisha hayo wakati akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu kutaka kujua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa Machi 2, mwaka huu alipotembelea mpaka huo wakati akiwa katika ziara ya siku sita mkoani Tanga.

Katika maagizo yake kwenye mpaka huo, Majaliwa aliagiza kudhibiti wageni wanaoingia katika njia za panya katika mpaka huo na kuhakikisha kila abiria anakaguliwa kikamilifu katika kudhibiti magendo na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaoambukizwa na virusi vya corona.

Sambamba na maagizo hayo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika ziara hiyo aliuagiza uongozi wa Kituo cha Pamoja mpakani hapo (OSBP) kutenga eneo maalumu ili ikibainika kuna abiria anahisiwa ana dalili za ugonjwa huo, ahifadhiwe kwa uangalizi zaidi, na kuwaagiza vijana wanaofanya biashara ya bodaboda, wawe waelimishaji wakubwa kwa abiria wanaowabeba katika mpaka huo.

Mark alisema kuwa hivi karibuni katika kituo cha pamoja cha mpaka wa Horohoro, kulikuwa na raia wa China aliyekuwa akitokea Mombasa nchini Kenya ambaye basi alilopanda (hakulitaja), alionesha kuwa na joto kali.

Kabla ya kushuka kwa ajili ya kukaguliwa, abiria wenzake walikuwa wanamzongazonga, hali iliyomfanya aingie hofu na kutoroka na kutaka kuingia nchini Tanzania kwa njia za panya.

Alisema baada ya kusikia taarifa hizo, uongozi wa wilaya walimtafuta, ambapo walimpata na kumrudisha upande wa Kenya.

Baada ya kupimwa iligundulika hakuwa na maambukizi ya corona, bali alikuwa amelewa.

WATU 11 wamekamatwa katika mpaka wa Horohoro uliopo kati ya ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Tanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi