loader
Picha

TBS yakagua maduka vitakasa mikono

SHIRIKA la Viwango (TBS) linaendelea kufanya ukaguzi madukani na viwandani, kuhakikisha bidhaa vikiwemo vitakasa mikono vilivyo sokoni vinavyouzwa, vinakidhi matakwa ya viwango.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TBS, Roida Andusamile alisema hayo jana akizungumzia ushauri wa watu mbalimbali kwamba shirika lifanye ukaguzi, kuhakiki viwango vya vitakasa mikono, kudhibiti uuzaji wa bidhaa zisizo na ubora katika kipindi hiki cha mlipuko wa corona.

“Kawaida ukaguzi hufanyika kila mara nchi nzima. Hii ni kazi yetu ya kila siku” alisema.

Aliongeza kuwa wakaguzi hununua sampuli na kuzipeleka katika maabara za TBS, kwa ajili ya kupima na kujiridhisha ubora wake.

Bidhaa zikibainika kuwa chini ya kiwango kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009, waziri mwenye dhamana ya viwanda na biashara, ana mamlaka ya kuamuru bidhaa husika kuondolewa sokoni na kusitisha uzalishaji.

Baada ya mlipuko wa corona nchini, kumekuwapo taarifa za kuwapo maduka hususani jijini Dar es Salaam yanayouza vitakasa mikono visivyokuwa na utambulisho kamili na kutengeneza hisia kuwa zinatengenezwa na kusambazwa kienyeji.

Mkazi wa Dar es Salaam (jina linahifadhiwa) aliliambia gazeti hili kuwa alikuta duka likiwa na vitakasa mikono visivyo na lebo kuonesha mchanganyiko uliotumika, tarehe ya mwisho ya matumizi, jina la mtengenezaji wala mahali vilipotengenezwa.

Andusamile alisisitiza watumiaji kuhakikisha wananunua vyenye maelekezo, yanayoonesha kuwa na alcohol isiyopungua asilimia 60 kwa mujibu wa kiwango cha kimataifa.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kemikali cha TBS, Gerald Magola alifafanua kuwa vitakasa mikono, si lazima vitengenezwe kwenye viwanda kikubwa.

WATU 11 wamekamatwa katika mpaka wa Horohoro uliopo kati ya ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi