loader
Picha

Lema kizimbani mashitaka 15

MBUNGE wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, akikabiliwa na mashitaka 15, likiwemo la kuhamasisha hisia hasi na kuweka mtandaoni taarifa za uongo.

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Mkuu, Monica Mbogo, kosa hilo la kuhamasisha hisia hasi kwa wananchi kwa nia ovu ni kinyume cha Kifungu 63B (1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 16 ya Mwaka 2002 wakati makosa mengine 14 ya kutoa taarifa za uongo kwa njia ya mtandao ili kupotosha umma ni kinyume cha Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandaoni Namba 14 ya 2015.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Consolate Singano ilidaiwa kuwa Lema alitenda makosa yote hayo Februari 29, mwaka huu eneo la Miembeni katika mji wa Manyoni wilayani Manyoni mkoani Singida.

Lema alikana makosa yote 15 na kuachiwa kwa dhamana hadi Aprili 15, mwaka huu, ili kutoa nafasi kwa upande wa mashitaka kukamilisha upepelezi wake.

Katika kesi hiyo namba 63/2020, Lema anatetewa na mawakili Mwiru Amani na Hemed Kulungu wakati upande wa mashitaka uliwakilishwa na Monica Mbogo, Rose Chilongola, Careen Mrago na Michael Ng’hoboko kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

WATU 11 wamekamatwa katika mpaka wa Horohoro uliopo kati ya ...

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Singida

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi