loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasiolipa kodi hatarini kupoteza viwanja

OPERESHENI maalumu dhidi ya wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi, imeanza kung’ata baada ya watu kadhaa kufikishwa mahakamani.

Walioshindwa kulipa, imeamriwa viwanja vyao viuzwe, kufidia madeni yao.

Katika operesheni hiyo iliyoanza Machi 6, mwaka huu, imeelezwa kwamba madai zaidi ya 700, yamefunguliwa mahakamani, huku Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikiendelea kusambaza nchini hati za madai zipatazo 6,800 zenye thamani ya Sh bilioni 20.

Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Ardhi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Msami ameliambia gazeti hili jana kwamba kwa Jiji la Dar es Salaam, Manispaa ya Ilala pekee mashauri 200 yamefunguliwa mahakamani.

Msami alisema siku hiyo ya mashauri, baadhi ya wadaiwa hususani wenye madeni ya kiasi kidogo cha fedha, walilipia mahakamani na kufanikisha takribani Sh milioni 12 kukusanywa.

Wengine waliahidi kulipa. Wengine ilitolewa amri mali zao zipigwe mnada.

Manispaa ya Kinondoni yapo mashauri 13 yenye thamani ya takribani Sh bilioni sita yatakayosikilizwa hivi karibuni.

Upande wa Kigamboni, Ubungo na Temeke, wizara inaendelea kusambaza hati za madai.

Mkoani Mwanza, mashauri 400 yameshafikishwa mahakamani na Mtwara, hukumu imetolewa kwa mashauri 100.

“Tayari dalali amepewa madaraka ya kuuza viwanja kufidia kodi ya ardhi na zoezi linaloendelea ni kwamba tunasambaza hati za madai nchi nzima,” alisema Msami Alisema itakapofika Aprili Mosi, wizara itauza viwanja husika kufidia pango la ardhi.

Wakati uhakiki ukiendelea kwa lengo la kubainisha idadi kamili ya wadaiwa, mkuu huyo wa kitengo alisema Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na madai mengi ya madeni ya kodi.

Alisema kupitia operesheni hiyo, wizara imebaini wapo wananchi wengi wanaomiliki ardhi kubwa wakiendesha shughuli mbalimbali zikiwamo za kibiashara, lakini hawalipi kodi.

Msami alisisitiza kuwa wizara lazima ifanye ukaguzi kwa kuwa baadhi ya wenye maeneo makubwa ni taasisi zilizoyakodisha kwa watu wengine kwa ajili ya kuendesha biashara na uwekezaji mbalimbali ikiwamo viwanda.

SERIKALI imesema inatoa bei halali ya madini inayonunua kutoka kwa ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi