loader
Picha

Mkurugenzi, wenzake 5 kortini hasara bil. 31/-

MKURUGENZI wa Kampuni ya Jaruma General Supplies Ltd, Lucas Mallya na wenzake watano, wamesomewa upya mashitaka 23 ya uhujumu uchumi yakiwemo ya kukwepa kodi, kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 31.48 na kutakatisha fedha.

Washitakiwa wengine ni Happy Mwamugunda, Prochesi Shayo, Geoffrey Urio, Mhasibu Tunsubilege Mateni na Mkaguzi wa Hesabu, Nelson Kahangwa. Walisomewa mashitaka hayo jana kupitia mahakama mtandao kati ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Gereza la Segerea.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa washitakiwa wote wanadaiwa kati ya Januari 2015 na Januari 7, 2020 jijini Dar es Salaam kwa pamoja waliongoza genge la uhalifu kwa nia ya kupata faida.

Alidai katika mashitaka ya pili hadi la saba, linalomkabili Mallya, anadaiwa Juni 3, 2019 Dar es Salaam alighushi kutengeneza stempu ya ushuru akionesha imetengenezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati si kweli.

Anadaiwa alitoa nyaraka hiyo ya kughushi TRA akionesha ni halali wakati akijua si kweli. Katika shtaka lingine inadaiwa Januari 7, mwaka huu, Chang’ombe A Temeke Dar es Salaam alikutwa na rola 93 za stempu zenye thamani ya Sh 80,516,000 alizochapisha bila kibali cha Kamishna wa Mapato.

Mshitakiwa huyo anadaiwa kati ya Januari 2016 na Desemba 31, 2019 Dar es Salaam, kwa kutengeneza stempu hizo za kughushi, alisababisha hasara kwa serikali ya Sh 15,241,075,169, akikwepa kodi kiasi hicho cha fedha.

Katika shtaka la saba, anadaiwa kutakatisha kiasi hicho cha fedha, huku akijua zinatokana na zao la kukweka kodi.

Mwamugunda ambaye ni Mkurugenzi wa Happy Imports Associates, anadaiwa Januari 2017 na Desemba 2019 bila kusajiliwa na Kamishna wa Kodi aliingiza katoni 413 za drostdy wine zenye thamani ya Sh 24,780,000 na mashitaka ya tisa anadaiwa kukwepa kodi ya Sh 9,584,401,393.

Mshitakiwa huyo anadaiwa katika kipindi hicho, alisababisha hasara ya Sh 9,584,401,393.

Pia anadaiwa kutakatisha kiasi hicho cha fedha, huku akijua fedha hizo zinatokana na zao la kukwepa kodi. Shayo anadaiwa Desemba 19, 2019 alisambaza bidhaa zilizowekwa stempu za kughushi, katoni 749 za mvinyo 75CL zenye thamani ya Sh 98,670,000, katoni 594 za drostdy hof 37.5CL zenye thamani ya Sh 12,002,000, katoni 14 za cousins 75CL14 zenye thamani ya Sh 16,240,000 katoni za Amalula 58 zenye thamani ya Sh 12,120,000, ambazo zote thamani yake ni Sh 139,032,000.

Washitakiwa hao wanadaiwa walikwepa kulipa kodi Sh 38,827,276 na kodi ya Sh 2,359,342,542.07. Katika mashitaka ya 15 na 16, wanadaiwa kuisababisha serikali hasara ya Sh bilioni 31.48 17 na kutakatisha fedha.

WATU 11 wamekamatwa katika mpaka wa Horohoro uliopo kati ya ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi