loader
Picha

Simba kujadili corona leo

UONGOZI wa Simba leo unatarajia kufanya kikao cha kujadili hali ya ugonjwa wa virusi vya corona, kabla ya hawajaanza kuwapangia wachezaji wa kikosi hicho ratiba ya kuanza mazoezi kujiweka tayari na michezo 10 iliyobaki ya kukamilisha msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kikao hicho kinafanyika huku nyota wa kikosi hicho wakianza kuripoti baada ya kumaliza mapumziko ya siku saba walizopewa kurudi nyumbani mara moja kisha kurejea na kuwekwa kwenye uangalizi maalumu kabla hawajapangiwa ratiba.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa kikosi hicho, Patrick Rweyemamu alisema kikao hicho kitawawezesha kupokea taarifa ya daktari wao, Yassin Gembe kuwapa hali halisi ya ugonjwa wa corona.

“Wachezaji walipewa mapumziko ya siku saba na zinaisha kesho (leo) wanatakiwa kuanza kuripoti, lakini kabla ya kuanza kupanga ratiba ya mazoezi kutakuwa na kikao cha uongozi wa timu, ambapo tutapokea ripoti kutoka kwa daktari wa timu majibu atakayotupatia kuhusu hali ya ugonjwa wa corona tutajua cha kufanya “alisema Rweyemamu.

Hatahivyo, Serikali hivi karibuni ilisimamisha shughuli zote za michezo hasa ile inayohusisha watu wengi ili kuwatinga watu na maambukizi ya ugonjwa huo hatari.

Meneja huyo alisisitiza hawezi kutoa ratiba ya mazoezi kwa sababu ligi hiyo ilisimamishwa kwa tahadhari ya kujikinga kusambaa kwa virusi vya corona ambapo hadi sasa watu 12 wameripotiwa kuambukizwa nchini.

Awali, wakati Simba wanawapa ruhusa walitoa taarifa kwa mashabiki wa kikosi hicho tahadhari watakazozichukua ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa viongozi na wachezaji wote wa timu hiyo namna salama ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Hata hivyo, wachezaji wa kikosi hicho Meddie Kagere na Clatous Chama wanategemewa kuwekwa karantini kwa siku 14 mara tu watakaporejea kutoka kwao ikiwa ni agizo na Rais Dk John Magufuli kuwa mtu yeyote anayetoka nje ya nchi atalazimika kufanya hivyo kujikinga na kusambaza virusi hivyo.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi