loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga, GSM zaacha watu njiapanda

MABINGWA wa kihistoria Yanga na wadhamini wao GSM, wameacha watu njiapanda kwa kushindwa kuzungumzia juu ya barua iliyokuwa ikitembea mitandaoni jana kuhusu kujitoa katika majukumu yaliyokuwa nje ya mkataba wao.

Tangu juzi kumekuwa na maneno ya hapa na pale kuhusu Yanga na GSM lakini awali yalitajwa kuwa ni uongo na kwamba yanazushwa na watu wasioitakia mema klabu hiyo lakini jana ikatoka barua inayodaiwa kuwa ni ya wadau hao.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na mmoja wa viongozi wa GSM, Faisal Mohamed , ilielezea namna walivyoshiriki kutatua changamoto zilizokuwa zinaikabili klabu hiyo, ikiwemo kusajili wachezaji wanne; Bernard Morrison, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima na Adeyum Salehe na makocha na kuwalipa mishahara.

Pia, kulipa bonasi mbalimbali, hoteli, tiketi za ndege za wachezaji na viongozi, madeni ya nyuma ya wachezaji na yote hayo walidai kufanya kwa mapenzi yao bila kujali gharama kubwa wanazotumia.

Mbali na hayo, barua hiyo ilisema katika kuelekea kwenye mabadiliko, walileta mtaalamu wa kuishauri timu hiyo na walitarajia kuleta timu kutoka barani Ulaya itakayojenga ushirikiano na Yanga kwa gharama za GSM, lakini kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi.

Wakaenda mbali zaidi na kusema watabaki kuwa mdhamini wa Yanga kimkataba kutekeleza yale yaliyo ndani ya mkataba na kuachana na yote waliokuwa wakifanya kwa mapenzi yao.

Gazeti hili lilimtafuta mmoja wa viongozi wa GSM ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Hersi Said kujua kama barua hiyo ni yao lakini mwenyewe alikuwa hapokei simu.

Pia, kwa upande wa msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kwa vile barua imeelekezwa kwa Mwenyekiti (Mshindo Msolla), basi atafutwe yeye atakuwa na majibu lakini alipotafutwa, simu iliita bila kupokelewa na baadaye ikawa haipatikani kabisa.

Na Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Fredrick Mwakalebela alisema yeye yuko Dodoma hivyo, hajui chochote.

Hata hivyo, baadhi ya wadau walitoa maoni yao akiwemo Ally Mayai aliyesema kuwa kama kweli barua ni ya GSM basi, viongozi wa Yanga wakae pamoja kumaliza tofauti zao.

“Wakae meza moja kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili wakilenga zaidi kwenye maboresho ya timu ipate matokeo mazuri,”alisema.

Kenny Mwaisabula alisema GSM wanapaswa kujua kuwa Yanga ni timu ya wananchi hivyo, maneno hayakosekani, wakae pamoja na kila mtu atambue maslahi yake.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi