loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tshishimbi awaita Simba SC

KIUNGO wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema mkataba wake na kikosi hicho unaelekea mwishoni, hivyo anakaribisha mazungumzo na timu yoyote inayohitaji huduma yake, ikiwemo Simba.

Kabla ya mchezaji huyo kuweka wazi hatma yake ndani ya timu hiyo, taarifa za chini zinadaiwa kwamba ameshaanza kufanya mazungumzo na mabingwa watetezi Simba.

Taarifa hizo zinasema Simba wanaonekana kupania kunyaka saini ya kiungo huyo kwa lengo la kumtumia kwa msimu ujao kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na ile ya kimataifa.

Akizungumza Dar es Salaam jana Tshishimbi, alisema mkataba wake na Yanga unamalizika Agosti na kwa sasa anasubiri timu itakayomfuata yenye dau kubwa asaini mkataba nao, kwani mpira ndio kazi yake.

“Mkataba wangu na Yanga unaisha mwezi wa nane na sasa nimesaliwa na miezi minne, hivyo nakaribisha mazungumzo na timu yoyote kutoka ndani na nje ya nchi inayohitaji huduma yangu lakini kikubwa nitakuwa naangalia maslahi ya fedha, ”alisema Tshishimbi.

Tshishimbi alikiri hadi sasa kuna viongozi wa timu ameanza kufanya nao mazungumzo na baadhi kwa njia ya simu wakionesha nia ya kutaka huduma yake.

Alisema kwa upande wa Yanga ameongea nao, lakini bado hawajakubaliana kutokana na mahitaji ambayo yeye kama mchezaji anatamani kuyapata.

Wiki iliyopita uongozi wa Yanga kupitia wadhamini wao GSM walianza zoezi la kuwaongezea mikataba wachezaji wao, ambapo hadi sasa wamefanikiwa kumalizana na kiungo raia wa Ghana, Bernard Morrison aliyeongezewa miaka miwili kuendelea kukitumikia kikosi hicho, huku wakibainisha kwamba wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha mazungumza na Tshishimbi.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi