loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bayern, Dortmund wakatwa mishahara kudhibiti corona

WACHEZAJI wa Bayern Munich ya Ujerumani na wakurugenzi wao wamekubali kwa kauli moja kukatwa kwa muda asilimia 20 ya sehemu ya mishahara yao.

Vigogo hao wa soka wa Ujerumani wamesema kuwa hatua hiyo wameifikia ili kusaidia wafanyakazi wengine wa klabu hizo kifedha wakati wa kipindi hiki cha matatizo ya virusi vya corona, ambavyo vimesababisha kusimamishwa kwa Bundesliga na ligi zingine za Ulaya.

Wiki iliyopita, wachezaji wa Borussia Monchengladbach walikuwa wa kwanza nchini kuacha mishahara yao.

Wachezaji wa Borussia Dortmund nao pia wako katika mazungumzo ili kukatwa mishahara yao, gazeti la Bild liliripoti.

Hakuna mechi za Bundesliga tangu Machi 8 kutokana na kuenea kwa virusi vya corona, ambavyo vimeikumba michezo duniani kote.

Wiki iliyopita, mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowski na mkewe walichangia Euro milioni 1 kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona.

Wachezaji wenzake, Leon Goretzka na Joshua Kimmich nao pia waliitisha michango kupitia jina la Tunapiga Teke Corona katika jitihada zao za kupambana na tatizo hilo.

Walichangia kiasi cha Euro milioni 1. Jumatano, Mamlaka ya Ujerumani ziliripoti kuwa kuna kesi 31,554 za maambikizi yavirusi vya corona huku tayari kukiwa na vifo 149.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: MUNICH, Ujerumani

1 Comments

  • avatar
    EDISON KATOTO
    08/04/2020

    Comment jamani tuombe mengi maombi kwa mungu aepushe hili janga la covid19 liishe na atusaidie awape madakitari bingwa uwezo waweze kufanikiwa katika jitihada za kutafti kinga/dawa ya kudhibiti ugonjwa huu. Yangu ni hayo 2 by edison boy

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi