loader
Picha

Waumini kufunga, kusali wiki 3 corona iishe

WAUMINI wa Kanisa la Watch Tower watafunga na kusali kwa siku 21 mfululizo, kuliombea taifa dhidi ya ugonjwa Covid-19.

Kanisa hilo lina waumini 70,000 katika nchi za Zambia na Tanzania.

Makao makuu ya kanisa hilo duniani yapo katika Kitongoji cha Kitika Kata ya Kasanga wilayani Kalambo mkoa wa Rukwa.

Kanisa hilo lilianzishwa miaka 105 iliyopita na kiongozi mkuu wa kiroho, Enock Sindani kutoka Marekani alikokuwa akiishi na kufanya kazi.

Kiongozi wa kanisa hilo, Jonas Siminga (80) akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu amesema kanisa hilo husherehekea sikukuu kubwa mbili kila mwaka, ambazo ni Siku ya Kuzaliwa Yesu Kristo inayosherehekewa Oktoba Mosi na Sherehe za Mwaka Mpya Aprili 14 kila mwaka.

"Hivyo katika maandalizi ya kuupokea Mwaka Mpya waumini wa kanisa hili upande wa Tanzania na viongozi wake watafunga kwa kusali kwa siku 21 mfululizo kuanzia Aprili Mosi hadi Aprili 21 kuliombea taifa ili Mungu aliepushe na hili janga la maambukizi ya covid-19. Tunaamini Mwenyezi Mungu ni muweza wa yote, atawaponya waliothibitika kuwa na maambukizi na kuwakinga ambao hawajaambukizwa," alisisitiza.

SERIKALI kupitia Ofi si ya Makamu wa Rais imeandaa rasimu ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi