loader
Picha

Wasiojulikana waharibu nguzo 30 Tabora

SHIRIKA la Umeme (TANESCO) mkoani Tabora limesema watu wasiojulikana wameharibu miundombinu ya umeme katika Kata za Kigwa na Igalula wilayani Uyui mkoani Tabora. Watu hao wamekata vishikizi vya nguzo za umeme, hali iliyofanya baadhi ya nguzo kudondoka na umeme kukatika.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Ofisa Usalama wa shirika hilo mkoani Tabora, Abeid Abeid amesema uharibifu huo umesababishia hasara ya zaidi ya Sh milioni 10, ikiwa ni gharama ya vifaa hivyo na hasara ya mapato kutokana na wateja kukosa huduma kwa siku mbili.

Nguzo zaidi ya 30 zinazopitisha umeme wa kilovolti 33 zilikatwa vishikizi, hivyo kuanguka na kusababisha wananchi wa Kata za Kigwa na Igalula na maeneo mengine wilayani humo kukosa huduma hiyo kwa siku kadhaa.

Abeid alitoa wito kwa wananchi wanaoishi karibu na nguzo zilizoathirika, kutosogea karibu na nguzo hizo wakati jitihada za kurejesha miundombinu hiyo katika hali yake ya kawaida zikiendelea kufanyika.

Mtendaji wa Kata ya Kigwa, Anastazia Elias alisema vitendo hivyo, vinarudisha nyuma maendeleo ya wilaya na taifa.

Ametaka wote wenye tabia za aina hiyo kuacha mara moja.

Diwani wa kata hiyo, Winston Msemo amesema baada ya kupata taarifa za uharibifu huo kutoka kwa wananchi na uongozi wa shirika hilo, wameanza operesheni kuwasaka wahusika.

Aliomba wananchi wa kata hizo, kutoa ushirikiano ili wahusika wote watiwe nguvuni.

KUTOKANA na maambukzi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi